MKUU wa
Mkoa wa Arusha John Mongela ameitaka mahakama ya Afrika ya haki za
binadamu ikafanye kazi zake kwa haki ili kuweza kupambana na matatizo
yaliyopo katika bara la Afrika.
Mongela ameyasema hayo alipokuwa akimwakilisha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu, katika hafla ya kuchagua na kuwaapisha majaji wapya wa Mahakama hiyo.
Ameahidi ushirikiano ili kufanikisha malengo ya nchi wanachama na mahakama katika kuimarisha haki za binadamu.
No comments :
Post a Comment