AFISA
Utawala wa kampuni ya ujenzi ya Makame Mwinyi Generals Supplies, Batuli
Bakari (39) na fundi umeme Said Abdallah (33), wamefikishwa katika
mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kusafirisha
dawa za kulevya.
Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Yusuph Abood mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Rita Tarimo imedai kuwa Mei 5, 2021 huko Mikocheni katika manispaa y Kinondoni jijini Dar es s Salaam washtakiwa walikutwa wakisafirisha gramu 194.93 za dawa za kulevya aina ya Heroine Hydrochloride.
Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza kesi za dawa za kulevya.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Juni 17, 2021 kwa ajili ya kutajwa kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika.

No comments :
Post a Comment