Tuesday, June 8, 2021

IGP SIRRO: SILAHA NA WATUHUMIWA WAMEKAMATWA ,

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, amesema kufuatia Operesheni ya wiki moja iliyofanyika katika Jiji la Dar es salaam, wamefanikiwa kukamata silaha za moto

pamoja na wahalifu waliokuwa wakijihusisha katika matukio mbalimbali ya kihalifu.

IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa kikao kazi cha kufanya tathmini, mafanikio na changamoto ambapo pia ameelekeza kufanyika kwa operesheni ya mwezi mmoja kwa nchi nzima ili kubaini mianya ya uhalifu na wahalifu.

Aidha, IGP Sirro amewaelekeza Makamanda wa Polisi nchini kufanya operesheni ya usalama barabarani dhidi ya magari yote yasiyokidhi vigezo vya kuwepo  barabarani ili  kuwahakikishia usalama watumiaji wa vyombo vya moto

No comments :

Post a Comment