Sunday, June 20, 2021

DAWASA KUMALIZA ADHA YA UPATIKANAJI MAJI JIJI LA DAR ES SALAAM IFIKAPO 2020

Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa DAWASA mkoa wa Makongo Mhandisi Edison Robert Venance akitolea kuhusu namna walivyojipanga kusambaza maji katika eneo la Goba pamoja na maeneo ya karibu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa. Mhandisi Cyprian Luhemeja akipata maelezo kutoka kwa Msimamizi wa Mradi wa DAWASA, Mhandisi Ishengoma Kakwezi kuhusu ujenzi wa tenki la maji la Tegeta A ambalo litakalokuwa na ujazo wa Lita milioni tano wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi na usambazaji wa maji kutoka Chuo Kikuu mkoani Dar es Salaam hadi Bagamoyo Mkoani Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja akitazama ujenzi wa tenki la maji la Tegeta A litakalokuwa na ujazo wa Lita milioni tano wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi na usambazaji wa maji kutoka Chuo Kikuu mkoani Dar es Salaam hadi Bagamoyo Mkoani Pwani.
Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja kishuka mara baada ya kumaliza ukaguzi wa ujenzi wa tenki la maji la Tegeta A 
Ujenzi wa tenki la maji la Tegeta A ukiendelea
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa. Mhandisi Cyprian Luhemeja akitazama ujenzi wa tenki la maji la Bunju litakalokuwa na ujazo wa Lita milioni tano wakati wa ziara yake ya kukagua miradi ya ujenzi na usambazaji wa maji kutoka Chuo Kikuu mkoani Dar es Salaam hadi Bagamoyo Mkoani Pwani.
Ujenzi wa tenki la maji la Bunju ukiendelea
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa. Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na wakandarasi wa ujenzi wa Tanki la kuhifadhia maji katika eneo la Vikawe unaotekelezwa chini ya mradi wa usambazaji wa  maji Makongo – Bagamoyo wakati wa ziara yake iliyokuwa na lengo la kupata taarifa za utekelezaji pamoja na maendeleo ya Miradi ya maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasa. Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara ya kukagua miradi ya ujenzi na usambazaji wa maji kutoka Chuo Kikuu mkoani Dar es Salaam hadi Bagamoyo Mkoani Pwani.

 Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemeja ametembelea na kuangalia kasi ya utekelezaji  mradi wa usambazaji maji

kutoka Bagamoyo hadi Makongo na kuwaahidi watanzania kuwa adha ya upatikanaji huduma ya maji kwa Jiji la Dar es Salaam kumalizika ifikapo 2022.

Ziara hiyo imelenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo unaohusisha ujenzi wa matanki makubwa ya kuhifadhi maji pamoja na ulazaji wa mabomba kwa umbali wa kilomita 1,426.

Akizungumza juu ya Utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Luhemeja amesema mradi unahusisha ujenzi wa matank matatu makubwa yakuhifadhi maji katika maeneo ya Vikawe, Tegeta ‘A’ na Bunju pamoja na ujenzi wa vituo viwili vya kusukuma maji.

"Kazi zingine zitahusisha ujenzi wa mabomba makubwa ya kusafirisha na kusambaza maji yenye kipenyo cha kuanzia inchi 10 mpaka 20 kwa umbali wa km 23.38 pamoja na ujenzi wa mabomba ya kusambaza maji yenye kipenyo kwanzia inchi 3 hadi inchi 8 kwa umbali wa km 1,195" aliongeza Luhemeja.

Afisa mtendaji mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema mkandarasi ana wajibu wa kuunganisha wateja zaidi ya 60,000 ili kumaliza changamoto za maji katika maeneo ya Bagamoyo, Mabwepande, Mivumoni, Madale, Wazo mpaka Changanyikeni ambapo mpaka sasa kazi imefikia asilimia 50.

“Mkataba huu tunagemea utakamilika mwezi Novemba na hadi sasa kazi inakwenda vizuri, kuanzia Julai,5 tutaanza kuunganisha wateja wa  Bagamoyo ambapo tunategemea kuanza na wateja 3500 ambao wataanza kunufaika na  mradi” aliongeza Mhandisi Luhemeja.

Mhadisi Luhemeja ameeleza miradi yote inayoendelea ni sehemu ya jitihada za Mamlaka za kuondoa changamoto ya maji Dar es salaam na kuahidi ifikapo 2022  DAWASA itatangaza kuisha kwa changamoto ya Maji Jijini Dar es salaam.
"Hadi sasa upatikanaji wa huduma ni asilimia 92 kwa Jiji la Dar es Salaam, haya ni mafanikio makubwa sana kwetu na tunahakikisha miradi hii ikikamilika itamaliza asilimia 8 iliyobaki " allimalizia Mhandisi Luhemeja

Kukamilika kwa mradi huu kutaenda kunufaisha wananchi wa maeneo ya Changanyikeni, Salasala, Kinzudi, Goba, Madale,    Tegeta A, Bunju, Mbweni, Mapinga, Mabwepande na Bagamoyo

Mradi huo ulianza kutekelezwa Novemba 2019, umegharimu kiasi cha Shilingi bilion 67 unatarajiwa kukamilika ifikapo Novemba 2021.

No comments :

Post a Comment