Monday, June 7, 2021

BENKI YA DUNIA YAIPA TANZANIA BILIONI 980 KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako akizungumza na wandishi wa habari baada ya kumaliza mazungumzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Afrika Dk.Taufila Nyamadzabo kikao hiko kimehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu kilichofanyika leo Juni 7,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu,akizungumza mara baada ya kuhudhuria Kikao cha Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Afrika Dk Taufila Nyamadzabo kilichofanyika leo Juni 7,2021 jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Afrika Dk Taufila Nyamadzabo,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako kikao hicho kimehudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu kilichofanyika leo Juni 7,2021 jijini Dodoma.

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Afrika Dk.Taufila Nyamadzabo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu mara baada ya kumaliza mazungumzo ya kikao hicho kilichofanyika leo Juni 7,2021 jijini Dodoma

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia,Prof.Joyce Ndalichako akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Afrika Dk.Taufila Nyamadzabo  mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika kikao kilichofanyika leo Juni 7,2021 jijini Dodoma

………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

BENKI ya Dunia imeidhinisha Fedha kiasi cha Dola Marekani milioni 425 sawa na shilingi

bilioni 980 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha miundombinu ya Elimu ya Juu nchini.

Hayo ameyasema leo Juni 7,2021 na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof Joyce Ndalichako mara baada ya kumaliza kikao kati yake na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia Anaesimamia Afrika Dkt. Taufila Nyamadzabo kikao kilichohudhuriwa pia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu

Prof.Ndalichako amesema kuwa Kiasi hicho cha fedha kimeidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Dunia Mei 27 mwaka huu ambapo kitasaidia kuongeza udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu kwa asilimia 30 na kuongeza walimu takribani 600.

Prof Ndalichako amesema ujio huo wa Mkurugenzi huyo wa Benki ya Dunia Ukanda wa Afrika ulikuwa wa kuangalia namna ambavyo Serikali ya Tanzania imekua ikitekeleza fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi ya elimu nchini.

Amesema Benki ya Dunia imekuwa ikiipatia Tanzania kiasi kikubwa cha fedha na asilimia 30 ya fedha hizo zinazotolewa zimekua zikielekeezwa na kutekelezeka kwenye miradi ya elimu.

” Niwashukuru sana ndugu zetu wa Benki ya Dunia, wamekua wakichangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa elimu nchini, kupitia ufadhili wao tumeweza kujenga Shule mpya, mabwalo, matundu ya vyoo na pia kukarabati shule kongwe kupitia mradi wa EP4R.

Lakini pia Benki ya Dunia walitupatia kiasi cha Sh Trilioni 1.1 kwa ajili ya mradi mkubwa wa kuimarisha elimu Sekondari ambapo Maarufu kama Sequip ambapo Shule 26 zinatarajiwa kujengwa nchi nzima kila Mkoa ukipata Shule shule ili kusaidia kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa Shule na kutembea umbali mrefu ,” Amesema Prof Ndalichako.

Amesema kwa sasa wanaendelea na mazungumzo ya kupata mradi wa kuimarisha elimu msingi na haswa kwenye eneo la teknolojia lengo likiwa ni kuzalisha kundi kubwa la vijana wenye uelewa mpana wa sayansi na teknolojia kuanzia ngazi za chini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Afrika Dk.Taufila Nyamadzabo ameihakikishia serikali kuwa wataendelea kushirikiana kwa karibu kuhakikishaTanzania inafikia lengo la kuwa na miundo mbinu sahihi na ya kutosha kwa ajili ya Elimu.

Ameongezea kuwa moja ya kipaumbele kikubwa kwa Benki ya Dunia kwa sasa ni kuimarisha upatikanaji wa wa rasilimali watu yenye ujuzi.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Ummy Mwalimu, ameahidi kuhakikisha fedha zinazotolewa na Benki ya dunia zinatumika kwa madhumini yaliyolengwa hususani, ujenzi wa madarasa yenye ubora katika shule za msingi na Sekondari, ujenzi wa matundu ya vyoo, maabara na mabweni.

Pia Waziri Ummy ameishukuru benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuhakikisha wanaimarisha ujenzi wa miundombinu katika shule za Msingi na Sekondari Nchini ambapo wameweza kusaidia kutatua changamoto za uhaba wa madarasa, matundu ya vyoo, maabara na maktaba.

” Mfano mwaka huu tumechagua zaidi ya wanafunzi 200 ambao waliacha Shule na kisha kurejea kusoma kupitia mfumo mbadala katika Taasisi ya Watu Wazima Tanzania (TEWW), lengo letu ni kuhakikisha kila mwanafunzi anapata haki ya kusoma,” Amesema Ummy.

 

No comments :

Post a Comment