Mkurugenzi
Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akitia saini
Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,NHIF na
KACU uliofanyika leo Jumatatu Juni 7,2021 Mjini Kahama
Mkurugenzi
Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts (kushoto) na Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF
Hipoliti Lelo wakitia saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima
baina ya benki ya CRDB,NHIF na KACU
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU), Emmanuel Cherehani akitia
saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,
NHIF na KACU . Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama, Mhe. Anamringi Macha
akishuhudia utiaji saini
Mkurugenzi
Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akibadilisha nyaraka
na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya
NHIF Hipoliti Lelo wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya Afya
kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani
(kushoto) akibadilishana nyaraka na Mkurugenzi mkuu wa biashara Benki ya
CRDB, Dkt. Joseph Witts wakati wa kutia saini Makubaliano ya Bima ya
Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Bwana Emmanuel Cherehani
(kushoto) akibadilishana nyaraka na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa
Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakati wa kutia
saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,
NHIF na KACU
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) , Emmanuel Cherehani
(kushoto) Mkurugenzi Mkuu wa Biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts
(katikati) na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa
Bima ya afya NHIF Hipoliti Lelo wakionesha nyaraka baada ya kutia saini
Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na
KACU
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati wa utiaji
saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,
NHIF na KACU
Kaimu
Mrajisi mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface akizungumza wakati wa utiaji
saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB,
NHIF na KACU
Mkurugenzi
mkuu wa biashara Benki ya CRDB, Dkt. Joseph Witts akizungumza wakati
wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki
ya CRDB, NHIF na KACU
Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wanachama Mfuko wa Taifa Bima ya afya NHIF
Hipoliti Lelo akielezea umuhimu wa bima ya afya wakati wa utiaji saini
Makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na
KACU
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Bwana Emmanuel Cherehani
akizungumza wakati wa utiaji saini Makubaliano ya Bima ya Afya kwa
wakulima baina ya benki ya CRDB, NHIF na KACU
Mkuu
wa Wilaya Kahama, Mhe. Anamringi Macha (katikati) akiwa na viongozi wa
Benki ya CRDB,NHIF na KACU katika hafla ya utiaji saini makubalinao ya
Bima ya afya kwa wakulima kati ya benki ya CRDB,NHIF na KACU
Na Kadama Malunde na Mavala - KahamaMkuu
wa Wilaya Kahama Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha ameshuhudia
utiaji saini wa makubaliano ya Bima ya afya kwa wakulima baina ya benki
ya CRDB,NHIF na Chama Kikuu Cha Ushirika Kahama (KACU)
Akizungumza
wakati wa utiaji saini huo leo Jumatatu Juni 7,2021 Mkurugenzi Mkuu wa
Biashara Benki ya CRDB Dkt. Joseph Witts amesema Benki ya CRDB imeamua
kuwashika mkono wakulima kwa kuwalipia gharama zote zinazohusu huduma za
afya na mkulima atalipia pindi atakapovuna mazao yake.
"Kupitia
Mpango huu unaolenga kurahisha huduma za bima ya afya kwa wakulima,
baada ya mavuno mkulima atarejesha malipo hayo bila riba yoyote baada ya
kuuza mazao yao ambapo tunaanza kuwapatia bima ya afya Wakulima 590 wa
tumbaku na wakulima 6800 wa pamba, jumla wakulima 7390", amesema
Dkt.Witts.
"Mkulima akiwa anadunduliza anaweka kidogo kidogo
katika benki yetu ya CRDB fedha zitakaa vile vile bila makato hata ya
shilingi moja", ameongeza Dkt. Witts.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa
Huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya NHIF Bw. Hipoliti
Lelo amesema licha ya NHIF kuwa na jukumu la kuwafuata wanachama
kukusanya michango na kuwapa matibabu wameamua kuwarahisishia wateja wao
kwa kuwapa njia rahisi ya kulipa michango yao akibainisha kuwa ukiwa na
Bima itagharamia matibabu ya familia nzima.
Kaimu Mrajisi wa
Mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface amewapongeza benki ya CRDB na NHIF kwa
huduma hiyo huku akisisitiza kuwa kumekuwa na changamoto za wakulima wa
tumbaku katika ulipaji wa mikopo kwa kuwa NHIF baada ya kutoa huduma
isije ikawa kilio kwa Benki ya CRDB.
"Tuweke mikakati mizuri namna mikopo itavyolipwa ili isije ikawa mzigo kwa Benki ya CRDB", amesema Hilda.
Mwenyekiti
wa Chama Kikuu cha Ushirika Kahama (KACU) Emmanuel Cherehani ameeleza
kufurahishwa na hatua zilizochukuliwa na Benki ya CRDB na NHIF katika
kusaidia wakulima na kuahidi kuwa atatoa ushirikiano wa hali ya juu ili
kufanikisha adhma ya mkulima kupata matibabu na kulipa malipo taratibu
na bila shida yoyote.
"Wakulima wote watakaokuwa wameandikishwa
kwenye mfuko huu tuhakikishe wana uwezo mzuri wenye kilimo kikubwa na
kidogo ili tuwavute wengi" ,amesema Cherehani.
Kwa upande wake
Mkuu wa Wilaya Kahama Mhe. Anamringi Macha amesema moja ya changamoto
kubwa katika wilaya ya Kahama ni hamasa na uelewa wa wananchi kujiunga
na bima ya Afya akibainisha kuwa kama mkuu wa wilaya amekuwa akipiga
kampeni kubwa ili kuhakikisha wananchi wanajiunga na bima ya afya kitu
ambacho ni kizuri na kinapunguza gharama za matibabu pindi wana familia
wanapoumwa.
Licha ya kuwapongeza CRDB,NHIF na KACU amewaomba waendelee kutoa hamasa kwa wananchi wajiunge na huduma za afya.
"Kwa
mazingira ya sasa magonjwa ni mengi na gharama za matibabu ni kubwa kwa
hiyo suala la kuwa na Bima ni muhimu sana. Naomba viongozi tuendelee
kuhamasisha wananchi kujiunga na bima ya afya kwani wapo baadhi ya
viongozi wamekuwa wakipotosha kuhusu huduma za afya kitu ambacho
kinapelekea wananchi kutokuwa na maamuzi sahihi," amesema Macha.
No comments :
Post a Comment