Na Christian Gaya wa HakiPensheni
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa orodha ya watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili waliosajiliwa hadi kufikia tarehe 31 Mei 2021. Orodha hii inatolewa kwa mujibu wa Kifungu cha 55(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.
Taarifa hiyo inasema aidha, kwa mujibu wa Kifungu cha 57 cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018 watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili ambao hawakuwa wamewasilisha maombi ya leseni Benki Kuu kabla ya tarehe 30 Aprili 2021 hawapaswi kuendelea kufanya biashara ya huduma ndogo za fedha hadi wawe wamepata leseni."Kuendelea kufanya biashara bila kuwa na leseni ya Benki Kuu ni
uvunjifu wa Sheria unaoweza kupelekea faini au kifungo kwa mujibu wa Kifungu
cha 16 cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018," taarifa hiyo inasisitiza.
Pia inaeleza ya kuwa Benki Kuu ya Tanzania itaendelea kutoa machapisho ya orodha iliyohuishwa ya watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la pili waliosajiliwa, ikiwemo orodha ya watoa huduma ndogo za fedha wa daraja la tatu na la nne.
Inasema ya kuwa Kwa maelezo zaidi, unaweza kuwasiliana na: Mkurugenzi wa Usimamizi wa Sekta ya Fedha, Benki Kuu ya Tanzania, S.L.P. 2939, Dar es Salaam au wasilisha barua pepe kwa jwsabi@bot.go.tz; vctarimu@bot.go.tz; nfmongateko@bot.go.tz; na dasasya@bot.go.tz
No comments :
Post a Comment