WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso ametembelea na kukagua Mtambo wa kusukuma maji (Pump Station No.03) eneo la
Maweni Arumeru. Mtambo huo ni miongoni mwa mitambo mitano ya kusukuma maji inayojengwa kwa ajili ya kupeleka maji katika Jiji la Arusha na viunga vyake.Kukamilika kwa ujenzi wa mitambo hiyo kutawezesha kuongezeka kwa uzalishaji na usambazaji wa maji katika Jiji la Arusha ambapo mahitaji ya sasa ya maji ni lita milioni 104 na uzalishaji wa sasa ni lita milioni 64.
Ukamilifu wa mradi huu mkubwa wa maji utamaliza kabisa tatizo la upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wakazi wa Arusha na viunga vyake.
No comments :
Post a Comment