Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akisaini kanuni za Uwekezaji
wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini huku Mkuu wa Kitengo cha
Huduma za Sheria, Lucy Saleko (kushoto) kutoka Wizara ya Maliasili na
Utalii akiwa pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mary Masanja (
kulia) wakishuhudia utiaji saini huo katika hafla hiyo iliyofanyika leo
Jijini Dodoma
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akizungumza kabla ya hafla
ya utiaji saini wa Kanuni za Uwekezaji katika maeneo ya Uhifadhi nchini
ambapo amesema kanuni hizo zinamruhusu Mwekezaji kumiliki eneo la
Uhifadhi kwa miaka isiyopungua miaka 25
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akizungumza kabla ya
hafla ya Utiaji saini wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimakakati katika maeneo
ya Uhifadhi ambapo amesema Kanuni hizo zitasaidia kuongeza Wawekezaji
katika sekta ya Utalii nchini.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (
TAWA) Meja Jen ( Mstaafu) Hamisi Semfuko akizungumza kabla ya hafla ya
utiaji saini Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi
ambapo amesema anatarajia Uwekezaji huo utaongeza mapato Serikalini kwa
vile unalenga Wawekezaji wakubwa
Mkurugenzi
wa Idara ya Wanyamapori, Dkt.Maurus Msuha ( kulia) akiwa na Mkuu wa
Kitengo cha Huduma za Sheria, Lucy Saleko wakimfutilia Waziri wa
Maliasili na Utalii wakati akizungumza wakati wa hafla ya utiaji saini
wa Kanuni za Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini
uliofanyika leo Jijini Dodoma
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan Kijazi akizungumza
kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro
wakati wa hafla ya Utiaji saini wa Kanuni za Kimkakati za Uwekezaji
katika maeneo ya Uhifadhi nchini ambapo amesema Wameanza na TAWA lakini
na TFS pia wana maeneo kama hayo ambayo yanahitaji kanuni hozo ili
Uwekezaji uweze kufanyika
Kamishna
Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi akiwa Kamishna Msaidizi wa Biashara
na Huduma za Utalii kutoka TAWA wakifuatilia utiani Saini wa Kanuni za
Uwekezaji wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi nchini uliofanyika leo
Jijini Dodoma.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro akiwa na Naibu Waziri wa
Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja akiwa kwenye picha ya pamoja na
Watumishi kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Watumishi
kutoka TAWA mara baada ya hafla ya utiaji saini wa kanuni za Uwekezaji
wa Kimkakati katika maeneo ya Uhifadhi uliofanyika leo Jijini Dodoma
………………………………………………………………………..
Wizara
ya Maliasili na Utalii imefungua milango mipya katika Sekta ya Utalii
nchini kwa kutia saini ya Uwekezaji wa kimkakati katika maeneo ya
Uhifadhi nchini kwa Wawekezaji wenye mitaji mikubwa wa kutoka ndani na
nje ya nchi.
Ameyasema
hayo leo Jijini Dodoma, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas
Ndumbaro wakati akitia saini kanuni za Uwekezaji wa kimkakati katika
maeneo ya Uhifadhi
nchini.
Waziri
wa Maliasili na Utalii amesema utiaji saini huo ni miongoni mwa njia
zitakazochangia kuongeza idadi ya Watalii kufika milion 5 na mapato
yapatayo bilion 6 ifikapo mwaka 2025 kupitia Sekta ya Utalii nchini.
Kwa
mujibu wa Kanuni hizo Wawekezaji wataweza kuwekeza katika maeneo ya
Mapori ya Akiba, Mapori Tengefu pamoja na Maeneo ya Wazi ya Wanyamapori
kwa miaka isiyopungua 25.
Akizungumza
kabla ya utiaji saini huo, Waziri Dkt.Ndumbaro amesema kanuni hizo
zimelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa ambao hata watalii watakaokuja
katika maeneo hayo ni Watalii wenye fedha nyingi ikiwemo watu maarufu
duniani.
Amesisitiza
kuwa kanuni hizo zitawezesha Wawekezaji hao kujenga mahoteli katika
maeneo ya Uhifadhi pamoja na kuweka miundombinu ya Utalii itakayosaidia
kuwavutia Watalii wengi kutembelea katika maeneo hayo.
Awali
amesema kanuni hizo ni mpya na uwekezaji huo katika maeneo hayo utakuwa
wa aina yake kwa vile umelenga Wawekezaji wenye mitaji mikubwa
watakaowavutia Watalii matajiri hali itakayopelekea pato la taifa
kuongezeka maradufu kupitia sekta ya utalii nchini.
Awali
Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ( TAWA) Meja
Jenerali ( Mstaafu) Hamis Semfuko amesema utiaji saini wa kanuni ni moja
ya hatua muhimu ya kupanua fursa zitokanazo na sekta ya utalii nchini.
”
Tuliamua kuja na wazo hili ili Wawekezaji wenye mitaji mikubwa waweze
kuwekeza katika maeneo ya Uhifadhi ambapo awali uwekezaji wa namna hii
ulikuwa hauwezekani” alisisitiza Mwenyekiti huyo Meja Jenerali ( Mst)
Semfuko
Kwa
upande wake , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Allan
Kijazi amesema atahakikisha Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, ( TFS )
nao wanasaini kanuni za namna hiyo nao waweze kuwavutia Wawekezaji
kuwekeza katika maeneo yao kwa vile wa maeneo yenye sifa kawa yalivyo ya
TAWA
No comments :
Post a Comment