……………………………………………………..
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas
Ndumbaro amewatoa hofu Watumishi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)
kutokana na hofu iliyotanda miongoni mwao na hivyo kuwahimiza
kuendelea kuchapa kazi kama kawaida.
Hatua hiyo inakuja
kufuatia kukabidhiwa taarifa ya Kamati iliyoundwa kuchunguza tuhuma za
ubadhirifu wa fedha pamoja matumizi mabaya ya Rasilimali Watu
zinazoikabili TTB
Ametoa rai hiyo
Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya
Wakurugenzi ya TTB mara baada ya kupokea taarifa ya Kamati ya
uchunguzi wa tuhuma hizo.
Waziri Dkt.Ndumbaro
amesema hatua ya maamuzi ya taarifa hiyo yataanza kuchukuliwa mwezi
Juni mwaka huu kutokana na sasa kukabiliwa na majukumu mengine.
Amesema mara tu
baada ya kuipokea taarifa hiyo naye amemkabidhi Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo, Dkt.Allan Kijazi kwa ajili ya kuifanyia kazi.
” Nakuagiza
Mkurugenzi Mkuu wa TTB itisha kikao na Watumishi zungumza nao watoe
hofu wahimize waendelee kuchapa kazi kama kawaida, kama Wizara tutatoa
maamuzi ya haki muda ukifika ” amesisitiza Dkt.Ndumbaro
Amesema majukumu ya msingi ya Bodi hiyo hayatakiwi yasimame yakisubiria hatua za maamuzi ya ripoti hiyo mpaka yatolewe.
Kufuatia hali hiyo,
Waziri Dkt. Ndumbaro amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa TTB kumchukulia hatua
Mtumishi yeyote ambaye hatatekeleza majukumu yake kwa visingizio vya
kusubilia hadi pale maamuzi ya ripoti yatakapotolewa.
Itakumbukwa mnamo
tarehe 10 April, 2021 Waziri wa Maliasili na Utalii,Dkt.Damas Ndumbaro
alimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa TTB, DevothaMdachi ili kupisha
uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu wa fedha pamoja na matumizi mabaya
ya Rasilimali watu zinazoikabili Taasisi hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu
wa TTB, Betrita Lyimo amesema atatekeleza maelekezo hayo ikiwemo
kuitisha kikao cha Watumishi wote wa Taasisi hiyo kwa lengo la
kuzungumza nao kwa kuwatia moyo na kuwasisitiza Wachape kazi .
No comments :
Post a Comment