Na Amiri Kilagalila,Njombe
Ili kukabiliana na hali ya udumavu kwa watoto mkoani Njombe,wananchi
wanaonufaika na mradi wa kunusuru kaya masikini (TASAF) kata ya Kidugala wilayani wanging'ombe wamelazimika kuanzisha mradi wa ufugaji wa samaki kwa ajili ya kubadili mlo na kukuza kipato.
Kitakwimu mkoa wa Njombe unashika nafasi ya pili nchini kwa kuwa na asilimia 49.6 za utapiamlo na udumavu,ambapo kutokana na uwepo wa changamoto hiyo baadhi ya kaya masikini wilayani wanging”ombe wameamua kuanzisha mradi wa ufugaji samaki ili kuwanusuru watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Baadhi ya wakazi hao kutoka kidugala akiwemo Atu Ng'ahala na Balton Kizumbe wameanzisha mradi huo ambao umekuwa na manufaa makubwa kwao na watoto wao.
“Tunaufurahia huu mradi kwasababu ni sehemu ya kitoweo kulingana na afya zetu za watu wa mkoa wa Njombe kwa hiyo tunawashukuru sana Tasaf kwasabu mrai umekuwa ni chachu hata kwa wengine”alisema Balton Kizumbe
Kutokana na uwepo wa tatizo la utapiamlo na udumavu kuathiri ndani ya kata ya Kidugala wilayani Wanging’ombe,diwani wa kata hiyo bwana Wilson Mbilinyi amesema katika lishe bora samaki ni muhimu kwa afya za watoto .
“Tuko sasa kwenye jitihada za kuhakikisha tunazalisha samaki kwa wingi ili tuweze kupambana na hili tatizo la udumavu “Wilson Mbilinyi
Bertha Nyigu ni Afisa lishe mkoa wa Njombe ambaye amesema maono ya wakazi wa mkoa wa Njombe kwa sasa ni kuona wanakuwa na watu wenye lishe bora hususani watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano.
“Mikakati imewekwa katika mambo makubwa ili kupunguza udumavu ikiemo.kupunguza kiwango cha udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano”alisema Betha Nyigu
Mradi wa kunusuru kaya masikini tasaf hapa nchini umekuwa ukitoa fedha taslimu kwa walengwa ambazo zimekuwa zikiwasaidia kujikimu kwa kuanzisha miradi midogo midogo inayowasaidia katika kuendesha familia na hata kuongeza kipato.
No comments :
Post a Comment