CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kimeiomba serikali kufanya mabadiliko
ya kimuundo kwa Chuo cha Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA) na kukipeleka katika Wizara ya kazi na Ajira.Hayo yamesemwa leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya wafanyakazi duniani inayofanyika kila Mei Mosi ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Mwanza yakihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Akitoa hotuba kwa upande wa ATE, Mwenyekiti wa Bodi Jayne Nyimbo amesema Chuo cha VETA kinatoa mafunzo ambayo moja kwa moja yanaenda kutoa ajira kwa vijana na hivyo ni wajibu kwa serikali kulifikilia hilo.
Amesema, VETA kwa sasa kipo chini ya Wizara ya Elimu lakini muundo huo unawanyima fursa VETA ya kukaa na kujadili masuala mbalimbali ya ajira kwa vijana pindi vyama vya wafanyakazi vinapokutana.
Aidha, ameiomba serikali kupunguza mlundikano wa kodi, tozo mbalimbali zinazoshindwa kuvutia wawekezaji na wafanyabiashara huku sheria za kazi ziendane na wakati uliopo kwa sasa.
No comments :
Post a Comment