Thursday, May 20, 2021

UDSM KUENDELEA KUTUMIA FURSA ZA WATAFITI KUTATUA CHANGAMOTO ZA KIJAMII

*************************************

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kimesema kitaendelea na kuhakikisha kinatumia fursa ya Watafiti mbalimbali ikiwemo wanafunzi,Wataalamu,ili kutatua changamoto mbalimbali za

kijamii ili kufikia malengo ya Serikali kukuza Uchumi na kuboresha Maisha ya Wananchi.

Ameyasema hayo jana Dar es salaam Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Prof Bernadeta Kilian wakati akitoa taarifa ya juu ya maadhimisho ya sita ya Wiki ya Utafiti na Ubunifu ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam inayotarajiwa kufanyika Mei 24 Mei 26 Mwaka huu kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni ambapo atakayefungua Waziri Mkuu Mhe Kasimu Majaliwa na kufungwa na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Joyce Ndalichako.

Hata hivyo alisema katika siku hiyo ya ufunguzi kutakua na Wazungumzuji Wakuu ikiwemo Mfanyabiashara Maarufu Mohammed Dewji atazungumzia nafasi ya sekta binafsi katika Utafiti na Ubunifu na Profesa Hulda Swai Mtafiti kutoka Chuo cha Nelson Mandela cha Arusha atazungumzia nafasi ya vyuo vikuu katika Ubunifu .

“Wiki hii hutoa fursa ya kuimarisha ushirikiano kati ya chuo kikuu cha dar es salaam na wadau mbalimbali kitaifa na kimataifa hivyo siku ya pili jumanne may 25 asubuhi kutakuwa na mjadala maalumu wa mashirikiano ya kimkakati utakaowashirikisha wadau kutoka katika sekta binafsi na vyombo vya habari”.

Pia maadhimisho ya utafiti na ubunifu itarumika kukumbuka michango iliyotukuka ya wanataaluma na wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam katika utafiti,ubunifu na ubadilishanaji wa maarifa. Hivyo katika sherehe za kufunga wiki ya maadhimisho hayo may 26 waziri wa elimu,sayansi na Teknolojia professor joyce Ndalichako atawatunuku tuzo watafiti na wabunifu bora katika makumbi 10 yaliyopangwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa ubunifu na ujasiriliamali Dkt. Ambrose Itika amesema wahitimu wa ubunifu na ujasiriliamali wanapatiwa nafasi ya kukaa chuoni mara baada ya kumaliza masomo yao na kuhatamiwa na chuo hivyo kupata fursa kukuza ujuzi katika uhalisia uliopo.

Aidha amesema wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam wanaohatamiwa wengi wao wameshinda tuzo mbalimbali nchi za nje na katika taasisi mbalimbali.

Sanjari na hayo amesema chuo kimekuwa na ushirikiano wa karibu na vyuo vya ndani pamoja na vya nje ya nchi ikiwemo Sweden.

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kinawaalika wadau wote wa elimu,jumuiya ya wahitimu,viongozi wa serikal,wadau wa maendeleo,mabalozi, viongozi wa kisiasa, viongozi wa vyama vya kiraia, waandishi wa habari na wanachi wote.

 

No comments :

Post a Comment