Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akipokea maelezo kutoka kwa
Meneja wa TANESCO Mkoa wa Dodoma Mhandisi Kenneth Boimanda wakati
Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea Banda la TANESCO katika maonyesho ya
teknolojia yanayo endelea katika Uwanja wa jamuhuri jijini Dodoma Leo
30 Mei 2021
Mhandisi
Erasto Chiswanu akielekeza wanafunzi wa Shule Sekondari ya Wasichana
ya Msalato jinsi Mradi wa Julius Nyerere unavyo tekelezwa wakati
wanafunzi hao walipo tembelea banda la TANESCO katika maonyesho ya
Teknolojia yanayo endelea katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) limepongezwa na kusifiwa kwa utekelezaji
thabiti wa Miradi mbalimbali ya Umeme ikiwemo miradi mikubwa ya
kimkakati na miradi midogo midogo ya usambazaji Umeme Nchini kote.
Pongezi
hizo zimetolewa na Mkuu wa mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka Tarehe 30
Mei 2021 alipotembelea banda la TANESCO katika maonyesho ya Teknolojia
yanayoendelea katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
Sambamba
na pongezi hizo, Mhe Mtaka ameshauri wataalamu wa Tehama wa Shirika
kushirikiana na vyuo vya elimu ya juu ili kuboresha mifumo ya utoaji
huduma ikiwemo huduma za ununuzi wa umeme wa LUKU na kuwezesha wateja
kununua umeme kisha umeme huo kuingie katika mita bila kumlazimu mteja
kwenda kuweka umeme katika mita.
Mhe.
Mtaka amesema pamoja na mambo mengi mazuri ambayo TANESCO imekuwa
ikiyafanya, ni vvyema Shirika likafanya ushirika na taasisi za elimu ya
juu ili kukuza ubunifu na kuwezesha wataalamu wa ndani kutumika katika
kutekeleza miradi mbali mbali bila kuhitaji wataalamu kutoka nje ya nchi
na ikiwezekana wataalamu wa Shirika waweze kufanya na kusimamia hata
miradi mingine mikubwa inayotekelezwa katika nchi jirani.
“Hii
nikutokana na uzowefu ambao wataalam wa TANESCO watakuwa wameupata
baada ya kukamilisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati” Alisema
Mhe. Mtaka
Mhe.
Mtaka aliongeza kuwa, Miradi ya umeme vijijini inatekelezwa kwa
weledi wa hali ya juu, ni vyema sasa TANESCO ikawezesha wataalam wake
kwa kushirikiana na Taasisi zingine za serikali kuanza kupeleka
wataamamu katika kandarasi za usimamizi wa miradi nje ya Nchi.
No comments :
Post a Comment