Na Mwandishi wetu,Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul ametoa wito kwa
mabalozi wa nchi mbalimbali zilizopo hapa nchini kulitumia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kujifunza lugha ya Kiswahili pamoja na kupata tafsiri sahihi ya nyaraka mbalimbali.
Mhe. Gekul ametoa wito huo alipokutana na Mabalozi kutoka nchi za Indonesia, Uturuki, Oman,Comoro Viet Nam na Cuba wakati wa Tamasha la Utamaduni wa Indonesia lililofanyika tarehe 29 Mei, 2021jijini Dar es Salaam.
"Serikali ilianzisha Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa lengo la kuendeleza lugha adhimu ta Kiswahili, hiki ndicho chombo chenye uwezo wa kutoa mafunzo sahihi ya lugha ya Kiswahili kwa wageni" - Mhe. Gekul
"Natoa wito kwa Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Prof. Dkt. Ratlan Pardede pamoja na Mabalozi wengine wote mlioko hapa na Maafisa wa balozi kuitumuia taasisi hii ya BAKITA kwa ajili ta mafunzo ya lugha ya Kiswahili, ukalimani pamoja na tafsiri za nyaraka mbalimbali" - Mhe. Gekul
Aidha Balozi wa Indonesia alimuhakikishia Mhe. Gekul kuwa Serikali ya Indonesia itaendeleza ushirikiano uliopo wa Kiuchumi na Kiutamaduni hususani katika eneo la Utalii wa Kiutamaduni.
No comments :
Post a Comment