INSPEKTA Jenerali wa Polisi Simon Nyakoro Sirro amemuapisha ACP S.R.Hamdun kuwa Kamishna wa Polisi katika ukumbi wa Mikutano Makao makuu ndogo jijini Dsm.
kiapo hicho kimekuja baada ya Mhe, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kumteua ACP Hamdun kuwa Kamishna na
Mkurugenzi wa Taasisi ya kupambana na kuzuia Rushwa(PCCB).IJP Sirro amempongeza CP Hamdun kwa weledi aliouonyesha katika utumishi wake ndani ya Jeshi la Polisi hasa alipokuwa Kamanda wa Polisi katika mikoa ya Ilala, Njombe, Kilimanjaro, Arusha na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum Dar es salaam.
Aidha CP- SALUM RASHID HAMDUN amemshukuru Mhe, Rais kwa kumuamini katika nafasi hiyo. Pia amelishukuru Jeshi la Polisi kwa nafasi alizopata na kuzifanyia kazi kwa weledi mkubwa. Amesema katika kazi mambo makubwa ni USIMAMIZI mzuri wa kazi, NIDHAMU na UADILIFU ni nyenzo muhimu katika utendaji wetu wa kazi za kila siku.
No comments :
Post a Comment