Kuhusu Equity Bank
Equity Bank Tanzania Limited ni taasisi ya kifedha inayofanya kazi nchini Tanzania chini Equity Group Holdings Plc iliyo na matawi katika nchi nyingine
za Kenya, Uganda, Sudan ya Kusini, Rwanda, Congo (DRC). Kwa sasa Equity ina matawi 15 na Mawakala zaidi 3,600 nchi nzima, ATM na huduma za kibenki kupitia Simu za mkononi na Intaneti.
*********************
Equity Bank (T) imeahidi kuendelea kutoa elimu ya fedha na mikopo nafuu kwa vikundi vya uwekezaji na uchumi maarufu kama Vicoba ili kuviongozea tija katika uzalishaji na hivyo kuviongezea vipato.
Akizungumza katika hafla ya kusherehekea miaka mitano ya kikundi cha Kikoba cha Faith Vicoba Group iliyofanyika katika hoteli ya Mbezi Garden jijini DSM, Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki ya Equity Tanzania Esther Kitoka alisema kuwa Benki hiyo imeleta sokoni mfumo maalum wa kigitali ujulikanao kwa jina la “Eazzy Kikundi” ili kurahisisha undeshaji na uwajibikaji wa vikundi hivyo vya uwekezaji. “Mpaka sasa Benki ya Equity tuna vikundi zaidi ya 1500 huku Vikundi 750 kati yao tukiwa tumeviunganisha katika nfumo maalum wa kidigitali yaani Eazzy Vikundi.
Hii ni platform yetu maalum inayowezesha vikundi kujiendesha kidijitali kwa kuwapa wana kikundi wote uwezo wa kuona muenendo wa akauti yao (in real time) kupitia simu zao za mikononi bila hitaji la kwenda benki kuomba statementi.
Hili linaisaidia sana katika kuweka uwazi katika uendeshaji wa kikundi na hivyo kuongeza uwajibikaji na kupunguza migongano isiyo na lazima. Kila muamala utakaopita kwenye akaunti ya kikundi utaendana na meseji (notification) kwa wanavikundi wote. Hii pia itahusisha namna bora ya kuruhusu miamala kidijitali bila hitaji ya kukutana mara kwa mara. Mambo yote kiganjani” alisema.
Bi.Kitoka pia alisema kuwa Benki ya Equity imedhamiria kwa vitendo kumkomboa mwanamke wa kitanzania kiuchumi na imeweka mpango dhabiti wa kufanikisha hilo na kuwa Benki ya Equity imeshatoa mikopo ya kiasi cha shilingi milioni mia mbili (200mn) kwa zaidi ya vikundi 100 nchi nzima. Vingi vikiwa ni vya kina mama na wajasiliamari wanawake.
“Benki pia imeshatoa mikopo ya zaidi ya shilingi bilioni tatu (3bn) kwa wajasiliamari wadogo wadogo zaidi ya elfu mbili nchi nzima. Hili ni kundi limalohusisha wafanyabiashara wadogo wakubwa kuanzia mama Lishe mpaka wamiliki wa viwanda vidogo vya uzalishaji vyakula vya mifugo. Tunaamini kuwa hili ni kundi muhimu sana kwa uchumi wa nchi yetu kwani ndio kundi linaloajiri watu wengi zaidi nchini. Tutaendelea kuwa nanyi Bega kwa bega ili kwa pamoja tufikie malengo tuliyojiwekea” alisema.
Akitoa nasaha zake kwa vikundi vya uwekezaji nchini, Bi.Kitoka aliwaasa wanavikundi hao kuongeza juhudi na kuzingatia Mshikamano, ubunifu, weledi na uwazi kwenye masuala ya Fedha na Uwekezaji.
“ Benki ya Equity inaahidi kuendelea kushirikiana nanyi katika shughuli zenu zote za kijamii kama hii ya leo. Tunalenga kukua nanyi kwa pamoja yaani – Growing together in Trust huku tukitoa mafunzo na Elimu ya Fedha na Uwekezaji kadri mtakavyohitaji – Tupo tayari kutoa madarasa ya bure ya jinsi ya kupanga mahesabu yenu vizuri – Bajeti, Akiba, Mikopo na maeneno mengi yote ya uwekezaji, iwe katika hisa au hata hati za serkali” alisema Bi.Kitoka.
No comments :
Post a Comment