…………………………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Waziri wa fedha na
mipango Dkt Mwigulu Nchemba anatarajiwa kufungua mkutano wa 26 wa
wanahisa wa benki ya CRDB unaotarajiwa kufanyika mei 22 mkoani Arusha
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa{AICC} huku gawiwo la wanahisa
likipanda kutoka shilingi17 ya mwaka 2019 na kufikia shilingi 22
kutokana na faida ya bilioni 165 waliyoipata 2020.
Hayo yalisema na
mkurugenzi mkuu wa benki hiyo Abdulmajid Nsekela wakati akiongea na
waandishi wa habari kuhusiana na mkutano huo utakaofanyika siku ya
jumamosi na siku ya ijumaa tarehe 21 ikiwa ni semina kwa wanahisa hao
ambapo alisema kuwa kuwa pamoja na kuwepo kwa janga la Corona mwaka
2020 mwaka huo ulikuwa wa mafanikio kwa benki hiyo kwani walijaribu
kupambana na athari za janga hilo kwa kusogeza huduma karibu zaidi na
wananchi na kuweza kupata faida ya shilingi bilioni 165 baada ya kodi
jambo ambalo halikuwahi kutukea miaka mingine.
“kila mwaka mkutano
mkuu wa wanahisa wa benki yetu unafanyika Mei isipokuwa mwaka jana peke
yake ambapo tulifanya mwezi wa sita kutokna na janga la Covid 19 na
mwaka huu tunaendelea na ratiba yetu na mkutanoutafanyika tarehe 22 na
wanahisa watapata fursa ya kuwa kwenye mkutano moja kwamoja lakini kwa
watakao shindwa kufika watashiriki kwa njia ya kidigitali,”Alisema
Nsekela.
Alifafanua kuwa
gawiwo kwa mwaka huu litapanda kutoka shilingi 17 ya mwaka 2019 na
kufikia shilingi 22 kuoka na mafanikio hayo lakini pia mikopo chechefu
kwa mwaka 2020 imepungua na kufikia asilimia 4.4 ukilinganisha na na
miaka mingine ambapo 2018 ilikuwa asilimia 9 na 2019 ikiwa ni asilimia
5.
“Niwahakikishie
wanahisa kuwa benki ina uimara wa kukabiliana na changamoto kwa maana ya
kukabiliana na majanga mbalimbali yanayoweza kutokea lakini pia
tutaendelea kuhakikisha tunawapa wanahisa wetu taarifa sahihi na kwa
wakati,”Alieleza.
Alisema mkutano huo
utakuwa na agenda mbalimbali kiwemo Agenda ya kuwachagua wakurugenzi wa
bodi ya wanahisa wa wa asilimia 1hadi 10 na wa wanahisa wa chini ya
asilimia 1 ambapo alitoa wito kwa wanahisa wa benki hiyo kuhudhuria kwa
wingi katika mkutano huo.
Aliendelea kusema
kuwa mkutano wa mwaka jana ulikuwa na ubunifu ambao kwa mwaka huu
ubunifu huo umeendelea kuongezeka na kwani benki hiyo imekuwepo kwa
miaka 24 lakini kila mwaka imekuwa ikijijenga na wanahisa wakiijenga. Na
pamoja na mkutano huo mwaka wa 2021 uaendelea ambapo kwa kota ya kwanza
wameweza kupata faida ya shilingi milioni 44.
No comments :
Post a Comment