CRDB
Benki kama taasisi inayotoa huduma za kifedha imeshiriki katika mjadala
uliolenga kuangalia mchango wa Teknolojia katika kuendeleza uchumi wa
Kidigitali . Katika Mjadala huo Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya CRDB
Bwana Bruce Mwile amesema Benki ya CRDB imetengeneza fursa nyingi kwa
watumiaji wake na sasa inafanya jitihada za kushirikiana na watoa
huduma za mitandao ya mawasiliano ya simu kuangalia namna bora ya
kupunguza gharama kwa wateja . "ukiangalia
zipo fursa nyingi sana katika Benki yetu ya CRDB, katika Uvumbuzi
tunaoufanya tunawajali watu wote hata wamachinga, walimu, watoto na hata
sekta mbalimbali, na ukitaka kujua kwamba sisi ni Benki inayosikiliza
wateja juzi tulizindua simu Banking na watu wakatoa maoni kwamba
tupunguze makato na tulifanya ivyo" Alisema Bwana Bruce Mwile.
Kwa
upande mwingine Mkuu wa Kitengo cha Mabadiliko endelevu ya Biashara
Benki ya CRDB Bi. Winfrida Wanyacha amesisitiza kuwa Benki ya CRDB
iko kwenye mchakato kufanya ushirikiano na kampuni za simu ili waweze
kushirikiana kwa pamoja kupunguza zile gharama ili kuweza kuwanufaisha
Watanzania wa kawaida wanaotumia huduma za kibenki.Maadhimisho ya Wiki
hii ya Uvumbuzi 2021 (INNOVATION WEEK 2021) yanaendelea LAPF TOWER
Makumbusho Jijini Dar Es Salaam.


Afisa
Mkuu Uendeshaji wa Benki ya CRDB Bwana Bruce Mwile (Katikati) wakati wa
mjadala uliolenga kuangalia mchango wa Teknolojia katika kuendeleza
uchumi wa Kidigitali kulia na kushoto kwake ni wadau wa sekta na
Taasisi nyingine.
Na Mwandishi Wetu.
Benki
ya CRDB imeshiriki katika Wiki ya Uvumbuzi kwa Mwaka huu 2021 , Mada
kuu ya mwaka huu ni “Ubunifu kwa Uchumi wa Kidijitali Stahimilivu na
Jumuishi ( Innovation for a Resilient and Inclusive Digital Economy ) ”.
Wiki
ya Ubunifu Tanzania imekua kwa kasi kutoka mwaka 2015 ikiwa na
wahudhuriaji karibu 500 hadi mwaka jana, 2020 ilipoudhuriwa na zaidi ya
watu takribani 7,000 na kuwa ya kitaifa zaidi. Wiki hii imetoa jukwaa
kwa wabunifu wengi kuonekana, wadau zaidi kuunda ushirikiano wa maana,
maarifa mengi ya kushirikishwa, mipango mingi ya ubunifu itakayoonyeshwa
na masuala muhimu yanayohusiana na sera kujadiliwa.
No comments :
Post a Comment