Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba na Bi.
Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda
ya AfrikaMashariki, wakisaini mikataba miwili ya mkopo wenye thamani
ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.4) kwa
ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Mto Malagarasi, Jijini Dar es
Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), na Bi.
Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, Kanda
ya Afrika Mashariki, wakibadilishana hati za mikataba miwili ya mkopo
wenye thamani ya dola za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni
323.39) kwa ajili ya kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa
Malagarasi, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania
(BoT), Jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel
Tutuba na Bi. Nnenna Nwabufo, Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya
Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki, wakionesha hati za mikataba ya mkopo wa dola
za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya
kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo iliyofanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw. Emmanuel Tutuba, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola
za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya
kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika Mashariki Bi. Nnenna
Nwabufo, akizungumza wakati wa halfa ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola
za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya
kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, hafla hiyo ilifanyika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
Ujumbe kutoka
Tanzania ukiongozwa na Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Bw.
Emmanuel Tutuba (wa pili kulia walioketi), wakiwa katika picha ya pamoja
na Ujumbe kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika ukiongozwa
na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa Kanda ya Afrika
Mashariki, Bi. Nnenna Nwabufo (wa tatu kulia walioketi), baada ya hafla ya utiaji saini hati za mikataba ya mkopo wa dola
za Marekani milioni 140 (takriban shilingi bilioni 323.39) kwa ajili ya
kufadhili Mradi wa kufua Umeme wa Malagarasi, katika ukumbi wa Benki
Kuu ya Tanzania (BoT), Jijini Dar es Salaam.
………………………………………………………………………….
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania imeingia mikataba miwili ya mkopo na Benki ya
Maendeleo ya
Afrika (ADB) wenye thamani ya dola za Marekani Milioni 140 kwaajili ya
kufadhili mradi wa kufua umeme wa malagarasi.
Akizungumza mara baada ya hafla
hiyo iliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Mhe.Emmanuel Tutuba amesema kuwa kati ya fedha
hizo,dola za Marekani Milioni 120 zitatolewa kupitia dirisha la banki ya
Maendeleo ya Afrika (ADB) na dola za Marekani milioni 20 kupitia Afrika
crowing Together Fund.
“Kusainiwa kwa mikataba hii
kutaongeza kiwango cha fedha kilichotengwa na Benki ya Maendeleo ya
Afrika kwaajili ya kufadhili miradi ya Sekta ya nishati nchini Tanzania
kutoka takribani dola za Marekani Milioni 325.19 hadi kufikia dola za
Marekani Milioni 465.19 (takribani shilingi trilioni 1.07). Amesema
Mhe.Tutuba.
Aidha Mhe.Tutuba amesema kuwa
Benki ya Maendeleo ya Afrika imeonesha nia ya kufadhili mradi mwingine
wa kufua umeme wa Kakono utakaokuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 87MW
ambapo maandalizi yanaendelea vizuri.
Amesema mradi wa Malagarasi
utahusisha ujenzi wa kituo kipya cha uzalishaji wa umeme wa gridi ya
49.5 MW chenye uwezo wa kuzalisha wastani wa GWh 181 za umeme kwa mwaka.
“Utekelezaji wa mradi unalenga
kuboresha usambazaji wa umeme katika mikoa ya magharibi mwa Tanzania ili
kuchangia mabadiliko ya kijamii na kiuchumi hapa nchini na kusaidia
katika jitihada za kupunguza umaskini”. Amesema Mhe.Tutuba.
Hata hivyo amesema mradi huo
utapunguza utegemezi wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia mafuta mazito na
kupunguza upotevu wakati wa umeme.
No comments :
Post a Comment