……………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Taasisi ya wakaguzi
wa ndani wa bara la Afrika {AFIIA} wameadhimia kufanya kazi kwa kutumia
viwango vya kimataifa kwa kuacha kutumia mbinu za kizamani kufanya
ukaguzi wakati teknolojia imekuwa pamoaja kuboresha utekelezaji wa
serikali katika mipango mbalimbali kwa kuzingatia maadili naufanisi ya
kufanya kazi.
Hayo yameelezwa na
Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Emmanuel Johanes wakati akifunga mkutano wa 7
wa wakaguzi wa ndani uliofanyika jijini Arusha ambapo alisema kuwa kwa
muda wa siki tatu za mkutano huo wamejadili mambo mbalimbali lakini
kubwa zaidi ni kuboresha mbinu za wakaguzi wa ndani hasa katika matumizi
ya teknolojia
Johanes alisema kuwa
wameangalia ni namna gani ambavyo teknolojia mbalimbali ambazo zimekuwa
zikitoka na kuendelea zinawafanya wakaguzi wawe na kazi ngumu ya
kuendana na kasi ya mabadiliko ambapo pia wameweza kuangalia agenda ya
ufisadi ambayo kwa Afrika ni tatizo kubwa.
“Tumeangalia ni kwa
namna gani wakaguzi wanajukumu la kusaidia kuboresha sera mbalimbali za
kudhibiti mifumo inayoweza kusababisha kuwepo kwa mianya ya ufisadi ili
tuweze kuzisaidia serikali zetu na hatimaye kuiondolea Afrika changamoto
hiyo,” Alisema Mwenyekiti wa Taasisi za Wakaguzi wa Ndani
Afrika,Emmanuel Johanes.
Alifafanua kuwa
wameona hayo waliyoyainisha kwa sasa ni kipaumbele kwa wakaguzi ambapo
wataendelea kuboresha zaidi kama walivyogundua tatizo kubwa ni
changamoto ya jinsi wakaguzi wa ndani wanavyofanya kazi na jinsi
wakaguzi wa nje wanavyofanya kazi na watazingatia zaidi kuboresha
mahusiano yao na kuangalia ni wapi wataweza kushirikiana kwa pamoja
kwani lengo lao ni moja la kusaidia serikali zao.
Kwa upande wake
meneja wa AFIA Kafaso Milinga ambaye pia ni mtendaji mkuu wa taasisi ya
wakaguzi wa ndani Tanzania alisema kuwa katika mkutano huo umeweza
kushirikisha wakaguzi kutoka nchi kumi ambao wamefika moja kwa moja
katika mkutano huo huku nchi nyingine zikishiriki kwa njia ya mtandao
ambapo dhumuni kubwa ni kuhakikisha wanawapa elimu ya kutosha wakaguzi
wa ndani, wakurugenzi na wafanya maamuzi mbalimbali ili waweze kutimiza
wajibu wao na kuongeza tija katika utendaji.
“Tumeangalia mada
mbalimbali zinazowahusu kwenye masuala ya utawala bora, uongozi,
Teknolojia ambayo inabadilika kila siku pamoja na masuala mengine
yanayowahusu,”Alisema Milinga.
Naye mmoja wa
washiriki wa mkutano huo Adam Kisema kutoka mamlaka ya maji Singida
alisema kuwa fani ya ukaguzi ni fani ambayo inabadilika kila siku hivyo
mkutano huo umewafanya kujiimarisha zaidi ambapo wameweza kubadilishana
mawazo.
No comments :
Post a Comment