Thursday, April 15, 2021

WAZIRI PROF MKUMBO AIHAKIKISHIA SERIKALI YA INDIA KUENDELEA KUWEKA MAZINGIRA BORA YA KIBIASHARA KWA WAFANYABIASHARA WAO

WAZIRI wa Viwanda na Biashara Prof, Kitila Mkumbo amesema Tanzania itendelea kushirikiana na India katika kuhakikisha mazingira bora ya kibiashara kwa wafanyabiashara pamoja na

kuendeleza za uhusiano wa kidplomasia kijamii na kiuchumi  katika nchi hizo.

Prof Mkumbo ameyasema hayo alipokuwa akishiriki katika mkutano kibiashara  kwa njia ya mtandao  kati ya India na Tanzania uliofanyika katika ofisi za Wizara zilizopo Mtumba jijini Dodoma.

Mkutano huo umelenga kujadiliana kuhusu fursa za biashara zilizopo, kuimarisha ushirikiano wa kibiashara, kubadilishana uzoefu na kuonyesha   maeneo muhimu ya biashara kati ya India na Tanzania.

Akiongea katika kikao hicho kilichohudhuriwa na Balozi wa India nchini Tanzania na Balozi wa Tanzania nchini India, pamoja na wenyeviti wa wafanyabiashara katika nchi hizo, Waziri Prof Mkumbo amewashauri wawekezaji kutoka India kuwa wakiwekeza Tanzania wataweza kuuza bidhaa na huduma zao katika nchi za Afrika Mashariki (EAC) na nchi za Jumuiya  ya Maendeleo kusini mwa Afrika(SADC) bila ushuru wa forodha na ukomo wa kiwango cha bidhaa kama ilivyo kwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania.

Akiwahimiza wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania, amesema kuwa Tanzania ni mwananchama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yenye ukubwa wa soko lenye idadi ya watu wasiopungua milioni 177. Pia Tanzania ni mwanachama wa Jumuiya ya Maendelea Kusini mwa Afrika yenye  ukubwa wa soko lenye idadi ya watu  zaidi  milioni 300. Vilevile Tanzania iko katika hatua za mwisho za kukamilisha majadiliano ya uanzishaji wa Eneo huru la Biashara Afrika litakalokuwa na ukubwa wa soko lenye idadi ya watu isiyopungua bilioni 1.5.

“Hivyo, kwa kuzingatia jinsi India ilivyoendelea katika Sekta ya Viwanda na Biashara, nawahimiza wafanyabiashara wa India kuja hususani wenye Viwanda kuja kuwekeza katika maeneo ya fursa zilizopo Tanzania hasa katika uongezaji wa thamani wa mazao ya kilimo, ngozi na madini”.

Aidha, Prof Mkumbo alizisihi taasisi za Serikali Tanzania na India kufanyia kazi vikwazo  vya kibiashara hususan vikwazo visivyo vya kiushuru (non- tariff barriers) ili kurahisisha upatikanaji wa bidhaa na huduma  baina ya nchi hizo huku wakizingatia ushindani katika biashara. Pi aliainisha kuwa  kwa sasa Tanzania inatekeleza Mpango wa “Blue Print” unaolenga kuboresha mazingira  ya biashara ili kuvutia biashara na uwekezaji.

“ Nafikiri hatutakubaliana kuwa mazao ya kilimo kutoka Tanzania kama viungo, mbaazi za kijani, korosho  na ufuta  ambavyo vinahitajika zaidi India  lakini havina soko la kuaminiaka," Amesema Prof Mkumbo.

Vilevile, Waziri amesema ili kutimiza azma hiyo ya kuendeleza biashara na uwekezaji baina ya nchi hizo, Serikali ya Tanzania na India imeanzisha Tume ya pamoja ya Biashara ( Joint Trade Commission (JTC)) inayokutana mara moja  ambapo mkutano wa JTC unatarajiwa kufanyika hivi karibuni nchini Tanzania.

 

No comments :

Post a Comment