Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis
akisalimiana na watumishi wa Wizara hiyo mara baada ya kuwasili ofisini
kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
wakifurahia jambo na Manaibu wake Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Mhe. Mwanaidi
Ali Khamis, Katibu Mkuu Idara Kuu ya Afya Prof. Mabula Mchembe na
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
(katikati) akimkabidhi zana za kazi ikiwemo Ilani ya Chama cha Mapinduzi
(CCM) kwa mwaka 2020-2025 Naibu wake anayeshughulikia Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (kushoto)
alipowasili ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma kulia ni Naibu Waziri
anayeshughulikia Afya Mhe. Dkt. Godwin Mollel.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis
akipokea zawadi ya kadi kutoka kwa Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya
Jamii Dkt. John Jingu kumkaribisha Naibu Waziri huyo ofisini kwake
Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis
akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya
Tano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kuwasili
ofisini kwake Mtumba jijini Dodoma.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima
(katikati)akiwa katika picha pamoja na Manaibu wake Mhe. Dkt. Godwin
Mollel (wa pili kulia), Mhe. Mwanaidi Ali Khamis (wa pili kushoto),
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Afya Prof. Mabula Mchembe (kulia) na kushoto ni
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii Dkt. John Jingu.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
………………………………………………………………………………
Na Raymond Mushumbusi, WAMJW Dodoma
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa kuongeza nguvu katika Wizara hiyo kwa kuzingatia umuhimu wa
Sekta ya maendeleo ya jamii.
Dkt. Gwajima
ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akizungumza na watumishi wa Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wakati
akimkaribisha Naibu Waziri anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis.
Dkt. Gwajima amesema
kuwa Maendeleo ya Jamii ni kitovu cha maendeleo ya taifa na kama Sekta
za maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii zikisimamiwa vizuri, sekta
zingine nitapata ufanisi na hivyo kuharakisha Maendeleo kwa Taifa zima.
“Sekta ya maendeleo
ya jamii ni mbeleko ya maendeleo ya taifa ni muhimu sana katika
kuchgangia sekta nyingine kuendelea na kukua katika kusaidia maendeleo
ya taifa kwa ujumla” alisema Dkt. Gwajima
Ameongeza kuwa
masuala ya maendeleo ya jamii yakikaa sawa matatizo mengi yanayowakumba
wananchi kama vile magonjwa hayatapata nafasi.
Dkt. Gwajima amesema
kuwa Jamii ikielimika ikielemika itatatua changmoto zinazoikabili
kutoka na elimu aliyoipata kutoka kwa wataalam wa Maendeleo ya Jamii na
Ustawi wa Jamii.
“Katika hili sekta ya
maendeleo ya jamii ikitumika ipasavyo watu wakaelimika na kujua vitu
vingi wataondokana na changamoto nyingi amabazo zinatatulika kwa jamii
kupata elimu ya kukabiliana na changamoto hizo kabla hazijaleta madhara
katika jamii” alisema Dkt. Gwajima
Kwa upande wake
Katibu Mkuu Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamaii Dkt. John Jingu
amemuhakikishia Naibu Waziri huyo kufanya kazi kwa kushirikiana ili
kuhakikisha matokea na matarajio ya Rais Samia Suluhu Hassan yanafikiwa.
Amesema Maendeleo ya nchi yanahitaji ubunifu na matumizi ya teknolojia na mabadiliko ili kuhakikisha wananchi hawanabaki nyuma.
Ameongeza kuwa hatua
ya Mhe.Rais kumteua Naibu Waziri anayeshughukia maendeleo ya Jamii ni ya
kujivunia sana na jambo linalofuata ni kuhakikisha maono ya Rais
yanatafsriwa kwa kwa vitendo.
“Niseme hii ni fursa
ya kutatua changamoto za Watanzania kwa viwango vinavyokubalika lakini
zaidi kutimiza matarajio ya Watanzania, alisema Dkt. Jingu.
Akizungumza mara
baada ya kukaribishwa Wizarani Naibu Waziri huyo anayeshughulikia
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Mwanaidi Ali Khamis
amesema kuwa atafanya kazi kwa ustadi na kwa kasi ili kuhakikisha kuwa
sekta anazosimamia zinakuwa na maendeleo na kutoa matokeo chanja na
yanayonufaishi jamii.
“Mimi nipo tayari
muda wowote na wakati wowote kuwasikliiza na kujifunza pia msiogope
tuelekazane kwa lengo la kupeleka mbele kazi za Wizara na kuwahudumia
wananchi” alisema Naibu Waziri Mwanaidi
Naibu Waziri wa
Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anayeshughulikia
Maendeleo ya Jamii Mhe. Mwanaidi Ali Khamis aliteuliwa na Rais wa
Jamnhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Samia Suliuhu Hassan Marchi 31,
2021 na kuapishwa April 1, 2021 kushika nafasi hiyo na kabla ya hapo
alikuwa Naibu Waziri wa Fedha.






No comments :
Post a Comment