Watuhumiwa
wakiwa wakitoka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo mara baada
ya kusomewa mashtaka mbele ya Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka
nane yakiwemo ya kuingiza na kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na
kibali kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Watuhumiwa
wakiwa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya
Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na
kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
Watuhumiwa
wakiwa wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya
Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na
kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano Tanzania (TCRA).
WATU
wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya
Mahakimu wawili tofauti kujibu mashtaka nane yakiwemo ya kuingiza na
kusimika vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kibali kutoka Mamlaka ya
Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) pamoja na kuisababisha Serikali ya
Tanzania hasara ya Sh. milioni.69
Katika
hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa serikali Ester
Martin akisaidiana na Adolf Ulaya na Adolf Lema imewataja washtakiwa
hao kuwa ni Hemed Hemed(22), Daud Kalombe(31) na Lucas Nkunguru(29) na
Jeremiah Laizer .
Washtakiwa walifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando.
Washtakiwa
wanakabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu kwa kuratibu
shughuli za kihalifu; kuingiza vifaa vya mawasiliano bila kuwa na kubali
cha TCRA; kusimika vifaa vya mawasiliano Tanzania na kuendesha mitambo
ya Mawasiliano bila kuwa na kibali.
Pia
kutumia vifaa vya mawasiliano bila kudhibitisha na TCRA; matumizi ya
kilaghai ya vifaa vya mawasiliano; kuisababisha hasara Serikali na TCRA
pamoja na kutakatisha fedha kiasi cha Sh 69, 690,000.
Mbele
ya Hakimu Chaungu imedaiwa kati ya Desemba Mosi, 2020 na Februari 22,
2021 katika maeneo Dodoma, Mbeya na Dar es salaam, washtakiwa walipanga
kujipatia faida kwa kuratibu shughuli za kihalifu.
Imeendelea
kudaiwa kuwa, katika siku na Mikoa hiyo, kwa matendo yao ya kihalifu
washtakiwa waliisababishia Serikali na TCRA hasara ya Sh. milioni 69
Aidha,
katika shtaka la kutakatisha fedha, inadaiwa katika kipindi hicho na
maeneo hayo hayo washitakiwa huku wakijua kuwa fedha hizo ni zao
tangulizi la uhalifu na matumizi ya kilaghai ya kukwepa tozo ambazo
zingelipwa kwa ajili ya kusambaza mawasiliano, walijipatia Sh. Milioni
69
Mbele
ya Hakimu Mmbando inadaiwa, kati ya Januari Mosi 2021 na Machi 6, 2021
katika mikoa ya Dodoma na Songwe, washtakiwa Jeremiah Laizer na Daud
Kambole wanadaiwa kupanga njama ya kujipatia faida kwa kuratibu shughuli
za kihalifu.
Shtaka
la pili, Februari 2, 2021 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Mwalimu Julius Nyerere, waliingiza vifaa vya mawasiliano bila kuwa na
leseni ya TCRA.
katika
shtaka la kutakatisha fedha, Laizer anadaiwa kutenda kosa hilo Februari
28, 2021 na Machi 5, 2021 katika eneo la Tunduma mkoani Songwe,
anadaiwa kujipatia fedha kiasi Sh 19, 734, 000 .
Pia wanadiawa kuisababisha Serikali hasara ya sh. Milioni 19.
Kesi zote zimeahirishwa hadi April 27, 2021 Washtakiwa wamerudishwa rumande.
No comments :
Post a Comment