Monday, April 12, 2021

VODACOM YASHIRIKIANA NA BRITAM INSURANCE KUZINDUA VODABIMA KUPITIA M-PESA

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni (katikati), Afisa Mtendaji Mkuu wa Britam Tanzania, Raymond Komanga (kushoto) na Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Zakaria Muyengi (kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima  (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima  kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huu umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni akizungumza kwenye  uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima  (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima  kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa TIRA, Zakaria Muyengi akizungumza kwenye  uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima  (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima  kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.

Afisa Mtendaji  Mkuu wa Britam Tanzania, Raymond Komanga ( kushoto )  akizungumza kwenye  uzinduzi wa huduma mpya ya VodaBima  (Bimika Kidijitali) itakayowezesha mteja kulipia bima  kwa simu ya mkononi kupitia M-Pesa. Uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar Es Salaam.

……………………………………………………………………………

Jukwaa la kidijitali linalowezesha upatikanaji wa huduma za bima kwa urahisi zaidi na za bei

nafuu kwa kushirikiana na kampuni ya Britam Tanzania.

  • Zaidi ya wateja milioni 13 wa M-PESA kupata Bima ya Magari kupitia simu zao
  • Aina zingine za huduma za Bima kuongezwa katika orodha ya huduma.

Tarehe 12 Aprili 2021. Dar es Salaam. Kampuni inayoongoza ya Teknolojia na Mawasiliano nchini, Vodacom Tanzania leo imetangaza kuzindua ‘VodaBima’ – huduma ya kidijitali itakayowapa wateja huduma ya bima kupitia M-Pesa na hivyo kuchochea matumizi ya huduma za bima kwa Watanzania kwa kutumia huduma hiyo kwa njia ya kidijitali.

Kulingana na ripoti ya Finscope 2013, matumizi  ya Bima nchini ilikuwa asilimia 13.0 ikiwa imeongezeka kutoka kutoka asilimia 6.8 2009. Pamoja na ukuaji huu, bima bado ni moja ya huduma za kifedha ambazo hazitumiki sana nchini. Sababu tofauti zinatajwa ikiwa ni pamoja na mwamko mdogo, kutokuaminika kwa huduma na vikwazo vya kupata huduma. Kama kampuni ya teknolojia iliyo na maono ya kuibadilisha Tanzania na kubadilisha maisha kupitia teknolojia, Vodacom inapenda kuziba pengo hili kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litarahisisha upatikanaji wa bidhaa za Bima.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa M-Pesa, Epimack Mbeteni alisema kuwa VodaBima ni nyongeza mpya kwa jalada la M-Pesa la bidhaa na huduma zote zinalenga kufanya ujumuishaji wa kidijitali nchini Tanzania uwe wa kweli.

“Kwa miaka 13 sasa, Vodacom M-Pesa imekuwa kichocheo muhimu katika ukuaji wa ujumuishaji wa kifedha nchini na kila wakati tunatafuta njia mpya za kushinikiza uchumi jumuishi wa kidijitali. Vodacom inakusudia kuziba pengo la upatikanaji wa huduma za bima kwa kutoa suluhisho la kidijitali ambalo litapunguza gharama na kuongeza upatikanaji wa bidhaa za Bima. 

VodaBima huwapa wateja fursa ya kujiwekea akiba ya Bima bila malipo katika mkoba wao wa VodaBima kwa mwaka mzima. Jukwaa la VodaBima litatuma taarifa za kumbukumbu kupitia SMS wakati Bima ya gari yako inakaribia kuisha.

Bwana Mbeteni ameongeza kuwa bidhaa hiyo mpya italeta huduma za bima karibu na wateja na kuongeza urahisi na upatikanaji wa huduma hiyo. Aliongeza kuwa huduma hiyo itakuza sekta ya bima nchini kwa ujumla. VODABIMA inatumia miundombinu bora ya teknolojia ya M-Pesa na mtandao mpana wa Vodacom ambayo inapatikana katika maduka Vodacom  nchini kote kuhakikisha usalama, urahisi wa upatikanaji wa huduma za bima.

“VodaBima ni huduma ya kwanza ya aina yake sokoni, huduma hii inarahisisha upatikanaji wa huduma za bima pamoja na mfumo wa kufanya madai. Kwa sasa tunatoa bima ya gari lakini tunapanga kuleta bidhaa zingine ili kukidhi mahitaji ya wateja na kwenda sambamba na mabadiliko ya soko,” alisema Mbeteni.

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania – TIRA, Zacharia Muyengi alisema kuwa kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma za bima kupitia simu za mkononi kutawanufaisha wateja zaidi kwani sasa watafahamu kwa kina huduma mbalimbali za bima zinazotolewa sokoni.

“Tunafanya kazi kukuza na kudumisha soko la bima linalojumuisha, lenye ufanisi, la haki na salama kwa faida na ulinzi wa wamiliki wa sera. Tunakaribisha matumizi ya teknolojia ya mawasiliano pamoja na ubunifu wa bidhaa  ili kuleta huduma hizi karibu na watu. Uzinduzi wa VodaBima ni hatua inayoelekea kuboresha huduma  ya bima nchini,” alifafanua Muyengi.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Britam Tanzania Raymond Komanga ambao wanashirikiana na Vodacom kusambaza huduma ya bima kupitia teknolojia ya kidijitali alisema kuwa matumizi ya teknolojia ya mawasiliano ya simu katika kupata bima ni hatua itakayofanya huduma hiyo ipatikane kwa watu wengi zaidi. Aliongeza kwamba huduma hiyo itasaidia kuhamasisha watu wengi zaidi kutumia huduma ya  bima na kukuza sekta hiyo kwa ujumla.

“Huduma ya VodaBima ni ya kimapinduzi kwa sababu italeta urahisi kwa wateja kupata huduma za bima kutoka kwa watoa huduma. Wateja hawatalazimika kutembelea kampuni za bima kwani wanaweza kupata huduma hiyo  kupitia simu zao za mkononi,” alisema Komanga huku akiongeza kwamba jamii itaelimika zaidi juu ya bidhaa na manufaa ya utumiaji wa huduma za bima.

Uzinduzi wa VodaBima ni sehemu ya mpango wa ujumuishaji kupitia teknolojia ya kidijitali ya kampuni ya Vodacom na hatua nyingine zaidi katika kuleta huduma karibu na wateja kupitia ubunifu  na teknolojia ya mawasiliano kupitia simu za mkononi.

“Tunataka wateja wetu wapate huduma ya bima iliyoimarishwa pande zote. VodaBima ni bidhaa ya ziada ambayo inaweza kupatikana kupitia zana (App) mpya ya M-Pesa ambapo wateja wanaweza kupata bidhaa zingine kama huduma za mikopo na akiba kama Songesha na M-Pawa,” alihitimisha Mbeteni.

Uzinduzi wa VodaBima ni sehemu ya mpango wa ujumuishaji  kupitia teknolojia ya kidijitali ya kampuni ya Vodacom katika kuleta huduma karibu na wateja kupitia ubunifu  na teknolojia ya mawasiliano kupitia simu za mkononi. 

 

No comments :

Post a Comment