#VIDEO: Benki ya CRDB, TIOB wazindua Kadi mpya kwa wanachama wa TIOB
Mkurugenzi
wa Idara ya Wateja Wadogo na Kati wa Benki ya CRDB, Boma Raballa
(katikati) akizungumza katika hafla fupi ya Uzinduzi wa Kadi ya
Uanachama wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB) uliofanyika leo Aprili
13, 2021 kwenye ofisi za Taasisi hiyo, zilizopo eneo la Kinondoni
Morocco, Dar es salaam. Kadi hiyo pia inaweza kutumika kama Kadi ya
Malipo ya kibenki ambayo inaweza kutumia kufanya malipo mbalimbali,
kutoa fedha kwenye ATMs au kwa Wakala yeyote wa Benki ya CRDB. Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB),Patrick Mususa na kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Kadi wa Benki ya CRDB, Farid Seif.
Baadhi ya Wanachama wa Taasisi ya Mabenki Tanzania (TIOB) na wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo.
No comments :
Post a Comment