wanafunzi wa shule ya sekondari ya shepherd wakisikiliza kwa makini .
Na Woinde Shizza, Michuzi Tv
WALIMU
wa shule mbalimbali wametakiwa kuwafundisha wanafunzi wao elimu ya
natharia na vitendo ili pindi wanapomaliza masomo yao na kwenda mtaani
waweze kujiajiri kirahisi na sio kutegemea kuajiriwa
Hayo
yameelezwa na mkurugenzi wa Taha Jackline Mkindi jana wakati
akikabibidhi komputa kumi
na vifaa vyake venye thamani ya Shilingi milioni 48 vilivyotolewa na
washirika wao ambao ni UNDP kwa ajaili ya kuwapatia wanafunzi wa shule
ya sekondari Shepherds iliopo katika Kijiji cha Manyire kilichopo katika
kata ya Mlangarine
Alisema
kuwa kazi ya TAHA ni kuhamasisha na kutangaza sekta ya horticulture
nchini ,lakini vilevile pia sekta hii inapendwa sana na vijana,na katika
kuhamasisha huku sasa hivi hatuangalii tu vijana ambao wanatoka vyuoni
lakini tunataka wale vijana ambao wanatoka kwenye msingi vijana ambao
wapo katika levo ya shule za msingi hadi wale waliopo katika shule za
sekondari pamoja na wale ambao kabla hawajafika vyuoni.
Alisema
kuwa wao kama TAHA wameanzisha mikakati mbalimbali kwa ajili ya
wanafunzi wa shule mbalimbali hapa nchini ,ambapo katika kuwagusa hawa
vijana ili waweze kuelewa kabisa na kupenda sekta ya kilimo kuanzia
wakiwa wadogo.
‘’chanzo
cha komputa hizi kuletwa hapa kama zawadi ni kwamba sisi kama Taha
tulikuja kutoa elimu ya kilimo cha mboga na matunda kwa wanafunzi hawa
wa shule hii ya sekondari ya shepherds baada ya kutoa elimu ,tulikuwa
tunawafatilia mara kwa mara n ahata mmoja wa washirika wetu alipokuwa
kututembelea ambaye ni UNDP tuliamua kumleta hapa ,alivyokuja na kuona
namna wanafunzi hawa wanavyofanya kilimo na kukielezea ,namna
uhamasishaji wa watoto hawa ulivyo ndio akaadi kuwapa komputa hizi
wanafunzi hawa ili waendelee kujifunza zaidi maswala ya kilimo “alisema
Mkindi
Alisema
kutokana na mambo ambayo wanayona wanafunzi hawa wanayafanya yamewapa
motisha zaidi ya kuendelea kutoa elimu kwa shule zingine na vijana
wengine kwani wanafunzi hawa wameonyesha wanauelewa mkubwa wa masomo ya
sanyansi na teknolojia jambo ambalo limewashangaza sana pia wana uelewa
wa mazao mbalimbali ya kilimo .
Aliwapongeza
walimu wa shule hiyo kwa namna wanavyoendelea kuwafundisha wanafunzi
hao na kusema kuwa wanawafundisha watoto hao jinsi ya kujiajiri pindi
wanapotoka shuleni hapo kwani wanakuwa na elimu ya maarifa na vitendo
kwa kilimo na jinsi wanavyoendelea kupewa elimu zaidi ndio itawasaidia
wao kuwa wadau wazuri wa kilimo hapo baadae,kwani kilimo ni mti wa
mgongo kwa maendeleo ya uchumi wa nchi yetu ya Tanzania .
Kwa
upande wake mmoja wawanafunzi wa shule hiyo Kennedy Lomboi aliishukuru
Taha kwa kuwapa elimu ya kilimo ambapo alisema kuwa wanaimani kabisa
pindi watakapo maliza elimu yao ya sekondari wanapoenda nyumba kusubiri
matokeo wataendelea kujiajiri kwa kufanya kilimo.
Aidha
aliishukuru UNDP kwakuona umuihimu wao na kutambua kazi wanazifanya za
kilimo wanapokuwa shuleni hadi wakaamu kuwapatia zawadi ya komputa
ambazo alisema kuwa zitawasaidia kuendelea kujifunza teknolojia
mbalimbali za kilimo kupitia mitandao mbalimbali
Kwa
upande wake meneja wa shule ya shepherds sekondari Lucy Moses
aliwashukuru Taha kwa kumleta mshirika wao ambaye ni UNDPaliyeweza
kuwapatia komputa kwa ajili ya wanafunzi waliopo hapo shuleni ambapo
aliwahaidi kuzitunza na kuzifanyia kazi wa lengo lililokusudia huku
akaiwasihi walimu wa shule zingine kujitahidi kutembelea TAHA na kupata
ujuzi ambao utawasadiia vijana kujifunza mbinu mbalimbali za kujiajiri
pindi wanapo maliza
shule na sio kutegemea ajira za serikalini.
No comments :
Post a Comment