Ujumuishi
wa huduma za fedha unasaidia kuongeza matumizi ya mifumo rasmi ya
kifedha na kuchochea shughuli za kiuchumi. Maendeleo ya kiteknolojia
yamesaidia taasisi za fedha kubuni mifumo jumishi ya utoaji huduma
ambayo imesaidia kwa kiasi kikubwa kufikia lengo la kusogeza huduma za
kifedha kwa watu wengi hususan waliopo vijijini.
Pamoja
na kupunguza gharama za miamala, huduma jumuishi za fedha zinafungua
milango ya fursa zinazoweza kuleta mapinduzi katika jamii. Taasisi za
fedha zimekuwa nyenzo muhimu kuwezesha hilo kwa kubuni njia mbadala za
kufikisha huduma kwa wananchi.
Benki
ya CRDB ilianzisha huduma ya SimBanking mwaka 2011 kwa lengo la
kurahisha upatikanaji wa huduma na kuwawezesha wateja kufanya miamala
yao ya kifedha popote walipo kupitia simu za mkononi, kwa kupiga
*150*03#.
Mwaka 2016, Benki ya CRDB ilianzisha huduma ya SimBanking App kupitia
simu janja (smartphones) ili kuendana na mahitaji ya wateja ambayo kwa
kiasi kikubwa yanachangiwa na ukuaji wa teknolojia.
Wachambuzi
wa masuala ya fedha wanasema kwa miaka yote iliyokuwa sokoni,
SimBanking imekuwa njia ya huduma za kifedha inayotegemewa zaidi katika
soko.
Kwa sasa Benki ya CRDB inatekeleza mpango wa miaka mitano (2018-2022)
ambao umejikita katika kutoa huduma za kidigitali kwa lengo la kuendana
na mabadiliko ya mahitaji ya wateja wao. Utekelezaji wa mpango huu
unachangia kuongeza nguvu katika jitihada za Serikali kutimiza Dira ya
Maendeleo ya 2025 kwani kupitia huduma za kidigitali Benki ya CRDB
itaweza kujumuisha Watanzania wengi zaidi.
Hivi
karibuni Benki ya CRDB ilizindua huduma ya SimBanking App iliyoboreshwa
zaidi inayowawezesha wateja kufungua akaunti ya Benki ya CRDB kwa
kutumia simu bila ya kwenda kwenye tawi kwa kutumia kitambulisho cha
NIDA na alama za vidole tu.
Maboresho
hayo ya huduma ya ‘SimBanking’ yamekuwa kivutio kikubwa kwa Watanzania
ambapo ndani ya mwezi mmoja wateja zaidi ya 2,000 wamefanikiwa kufungua
akaunti kupitia simu zao, huku miamala zaidi ya milioni 2.5 ikifanyika
ndani ya kipindi hicho.
“Ubunifu
huu waliokuja nao Benki ya CRDB ni wakupongezwa sana, mwanzoni nilikuwa
na shaka inawezekanaje lakini nilipo pakua SimBanking App katika simu
yangu niliweza kufungua akaunti kwa hatua chache tu,” anasema Juma Mlala
mjasiriamali wa Gairo, Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Abdulmajid Nsekela, anasema Benki ya
CRDB imejidhatiti kuwawezesha watanzania wengi zaidi kupata huduma za
fedha kupitia mifumo ya kidijitali ikiwamo SimBanking.
Awali
kabla ya ujio wa huduma ya SimBanking, Watanzania wanaoishi vijijini
walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma za kifedha.
“SimBanking App imekuwa na msaada mkubwa kwa Watanzania hususani
wanaoishi vijijini kwa kuwa kwa sasa huduma za kifedha zinapatikana
viganjani mwao kupitia app hiyo,” alisema Nsekela.
David
Machumu, mwalimu ambaye ana akaunti ya CRDB katika wilaya ya Malinyi,
mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa wanufaika wa SimBanking.
Akitoa ushuhuda wanamna ambavyo SimBanking imesaidia kuboresha maisha
yake, Machumu, amesema miaka ya nyuma kabla ya kujiunga na SimBanking
ilikuwa inamlazimu kila mwisho wa mwezi kusafiri mpaka wilaya ya
Ifakara, umbali wa kilometa 108 kuangalia kama ameingiziwa mshahara wake
kwenye akaunti.
“Kabla
ya SimBanking ilikuwa inatugharimu sana linapokuja suala la pesa na
muda,” alisema Machumu. Kupitia SimBanking Machumu kwa sasa hana haja
ya kusafiri umbali mrefu kwa kuwa anaweza akatumia simu yake ya
kiganjani kuangalia kama ameingiziwa mshahara wake na pale anapohitaji
pesa taslimu hufanya miamala kwa CRDB Wakala waliopo wilayani humo.
Huduma
ya SimBanking imesaidia sana kubadilisha mtazamo wa Watanzania wengi
juu ya upatikanaji wa huduma za kibenki kwani hivi sasa takribani
asilimia 95 ya huduma hupatikana kiganjani.
Akielezea
huduma zinazopatikana kupitia SimBanking, Nsekela amedadavua kuwa mbali
na kuwawezesha wateja kufungua akaunti wenyewe, SimBanking sasa hivi
inatoa wigo mpana wa huduma za benki hiyo ikiwamo kuomba mkopo, kulipa
bima, kuhamisha pesa, kulipia manunuzi, pamoja na huduma ya kutoa fedha
kupitia matawi, CRDB Wakala na ATMs.
Sanjari
na huduma hizo, mteja pia anaweza kufanya malipo ya kodi za Serikali
kwenda Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), malipo ya bandarani kwenda
mlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni
(Brela) pamoja na bili za umeme na maji.
“Uwepo
wa huduma zote muhimu za kibenki kupitia SimBanking, unaifanya kuwa
benki kiganjani na ndio maana tunasema ‘Benki ni SimBanking’,”
ameongezea Nsekela huku akibainisha kuwa kipaumbele cha Benki ya CRDB
ni kutoa huduma bora na zinazopatikana kwa urahisi.
Wakati wa uzundizi wa maboresho ya SimBanking, Waziri wa Mawasiliano na
Teknoljia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile alionyesha matumaini
makubwa kwa huduma hiyo kuchangia katika ajenda ya nchi ya kuongeza
ujumuishi wa kifedha.
Ndungulile
aliitaka Benki ya CRDB kuendelea kutoa elimu kwa Watanzania juu ya
faida ya mfumo huu wa SimBanking katika kurahisisha upatikanaji wa
huduma, huku akiwahamasisha wananchi kujiunga na kuanza kufurahia huduma
hiyo.
No comments :
Post a Comment