Wednesday, April 14, 2021

SERIKALI YAKUSUDIA KUTATUA CHANGAMOTO KWA WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

……………………………………………………………………………………
 
Wizara ya Madini kupitia Idara ya Huduma za Sheria imeongoza kikao kazi chenye lengo la

kujadili changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utekelezaji wa Mkataba (framework agreement) baina ya Serikali na Kampuni ya Uchimbaji Mkubwa wa Madini ya Barrick kilichofanyika leo tarehe 14 Aprili, 2021 katika ukumbi wa mikutano wa wizara Mtumba jijini Dodoma. 
 
Kikao hicho kilichoongozwa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Madini (DLS), Edwin Igenge kimehusisha Wataalamu wa Sheria kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini, Wizara ya Katiba na Sheria, Meneja wa Kampuni ya Barrick nchini, Mwanasheria wa Barrick, Wataalamu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Wataalamu kutoka kwa Mwanasheria Mkuu  wa Serikali.
 
Aidha, maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho yatawasilishwa kwa uongozi wa juu wa Wizara mapema ili yaweze kufanyiwa kazi na hivyo kuondoa changamoto zinazojitokeza ktika utekelezaji wa makubaliano yaliyofikiwa  baina ya Serikali na Kampuni hiyo ya uchimbaji wa madini.
 
Kikao hiki ni mwendelezo wa juhudi za Serikali katika kuvutia uwekezaji nchini kwa kusikiliza na kutatua kero wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

 

No comments :

Post a Comment