Na Lusungu Helela-Morogoro
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro ameiagiza Menejimenti ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi kuhakikisha inawarejesha Faru ambao walitoweka miaka ya 80 kutokana na kukithiri kwa vitendo vya ujangili katika Hifadhi hiyo.
Akizungumza
leo mkoani Morogoro na Menejimenti ya Hifadhi hiyo, Dkt.Ndumbaro
amesema kwa kuwa Faru hao walikuwepo kipindi cha nyuma lakini tatizo la
ujangili lilipelekea faru hao kutoweka kabisa.
Amesema
Hifadhi hiyo kwa sasa ina Wanyamapori wakubwa wa nne na sio watano
ambao ni Simba, Tembo, Nyati na Chui. “Kwanini Faru hawapo katika
Hifadhi hii, Je mazingira sio rafiki kwao” alihoji Dkt.Ndumbaro
”
Katika uongozi wangu lazima nihakikishe Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
inakuwa “Big Five na sio Big Four ” , Menejimenti nataka kuwaona faru
katika Hifadhi hii kwani naamini wanaweza kuishi” alisisitiza
Dkt.Ndumbaro.
Amesema
ikolojia ya Hifadhi yaTaifa ya Mikumi inaruhusu Faru kuweza kuishi
katika eneo hilo ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma waliishi, Hivyo
kurejeshwa kwao kutasaidia Hifadhi ya Mikumi kuwa Hifadhi bora zaidi kwa
vile itakuwa imesheheni kiu ya Watalii wenye matamanio ya kuona
Wanyamapori wakubwa wote katika Hifadhi hiyo
Ameagiza
kuwa mara baada ya faru hao kurejeshwa katika Hifadhi hiyo ni lazima
ulinzi uimarishwe maradufu ili kosa lililotokea kipindi cha nyuma
liisijirudie.
”
Hakikisheni mnawafunga vifaa maalum vitavyowasaidia kuangalia mienendo
yao ili kuwahakikishia usalama wao” alisisitiza Ndumbaro
Amesema
kurejeshwa kwa faru hao ni ishara tosha kuwa tatizo la ujangili nchi
nzima umepungua kwa asilimia 90 hivyo kuna usalama wa Wanyamapori wote
wakiwemo faru watakaoletwa.
Kwa
upande wake, Mtafiti wa kutoka Taasisi ya Utafi wa Wanyamapori
Tanzania( TAWIRI) Dkt. Gabriel Ottawa amesema inawezekana faru
watakaorejeshwa wataweza kuishi vizuri kwa vile kipindi cha nyuma faru
hao walikuwepo katika Hifadhi hiyo
Ameahidi
mbele ya Waziri kuwa watafanya kila liwezekanalo kwa kufanya tafiti
mbalimbali kabla ya kuwaleta faru hao ili kujua changamoto pamoja na
kuzitafuta ufumbuzi wa namna faru hao wakishaletwa waweze kuishi kwa
usalama ili waweze kuendeleza kizazi katika Hifadhi hiyo.
No comments :
Post a Comment