
****************************************
Na Munir Shemweta, MISUNGWI
Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi ameitaka halmashauri ya
wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza kuhakikisha inapanga na kupima maeneo
yanayopitiwa na miradi ya kimkakati ya treni ya Mwendokasi (SGR) na
Kivuko cha Kigongo katika halmashauri hiyo mkoani Mwanza.
Akizungumza wakati wa
ziara yake ya kutembelea maeneo ya miradi ya upimaji katika maeneo ya
miradi hiyo leo tarehe 1 Februari 2021 Lukuvi alisema, hakuna kuendeleza
maeneo yanayopitiwa na miradi ya SGR na Kivuko cha Kigongo mpaka maeneo
hayo yatakapopangwa mpango wa matumizi bora ya ardhi.
” Maisha lazima
yabadilike na msinyang’anye wananchi maeneo yao bali maeneo hayo
yapangwe na kupangiwa matumizi yatakayoendana na hadhi ya miradi”
alisema Lukuvi.
Alisema, halmashauri
ni mamlaka ya upangaji hivyo Misungwi inapaswa kuzuia kuendelea kwa
ujenzi katika maeneo hayo mpaka yapangwe kwa lengo la kupandisha hadhi
na kuwa mji wa kisasa (modern city) ambapo alisisitiza kuwa haiwezekani
kuacha eneo linaloweza kuhudumia takriban nchi tano likaachwa kiholela.
” Zuieni maendezo
yote kandokando ya daraja ili muyapange vizuri na wanaotaka kuendeleza
mhakikishe wanaendeleza yale yanayoshabihina na mradi” aliongeza Waziri
wa Ardhi.
Aliongeza kwa kusema
kuwa kiasi cha shilingi milioni 300 ilizokopeshwa halmashauri ya wilaya
ya Misungwi na Wizara ya Ardhi kwa ajili ya mradi wa kupanga, kupima na
kumilikisha ziendelee kubaki kwa ajili ya kupanga maeneo ya mradi na
kubainisha kuwa, hata halmashauri hiyo ikihitaji wataalamu kutoka
wizarani kusaidia mradi wa upimaji katika eneo hilo basi inaweza
itapatiwa.
“Lazima misungwi uwe
mji maarufu mtu akitaka kuja kulala aje maana hili ni daraja la
kimkakati litakalohudumia takriban nchi tano, tunataka satelite city
iliyopangwa na itakayokuwa na huduma zote za msingi zenye hadhi
inayofanana na mji huo.
Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi alitembelea eneo la mradi
wa upimaji katika kitongoji cha Kigongo kilipo kivuko cha Kigongo
(Kigongo Ferry) pamoja na eneo la kimkakati la Fella inapopita treni ya
Mwendokasi ya SGR.
Mkuu wa Idara ya
ardhi katika halmashauri ya wilaya ya Misungwi Fredrick Nyoka alisema,
tayari idara imeanza kazi ya upangaji na kupima maeneo yanayopitiwa na
miradi ya SGR na Kivuko cha Kigongo na tayari baadhi ya wananchi
wameshalipwa fidia na Mamlaka ya Bandari Tanzania huku Shirika la Reli
likitarajiwa kumaliza kuwalipa fidia wananchi mwisho wa wiki hii.
No comments :
Post a Comment