Na Woinde Shizza, Michuzi Tv
WANANCHI
wanaomiliki ardhi katika kijiji cha Kiseriani kata ya Mlangarini,
halmashauri ya wilaya ya Arusha, mkoani Arusha wamejitokeza kwa wingi
kuchangamkia fursa ya urasimishaji unaofanyika katika maeneo yao, wakati
wa utekelezaji wa mradi wa urasimishaji Ardhi katika kijiji hicho,
mradi unaotekelezwa kupitia wataamu wake wa ndani.
Wakizungumza
na mwandishi wa habari jana, walipotembelea eneo la Kiserian, wamiliki
hao wa ardhi, wamekiri kuchangamkia fursa hiyo, na kudai imekuja wakati
muafaka na kupongeza juhudi za halmashauri hiyo, kwa kutekeleza mradi
wa urasimishaji ardhi katika kijiji cha Kiseriani na vitongoji vyake,
zoezi lililoshirikisha wananchi wote katika hatua zote.
Katibu
wa kamati ya Urasimishaji Kitongoji cha Losirwai, Lomayan Maiko Mollel,
ameweka wazi kuwa wananchi wa Kiseriani, wameupokea mradi wa
urasimishaji kwa matumaini makubwa ndio maana wamejitokeza kwa wingi,
kurasimisha maeneo yao waliyokuwa wanayamiliki kihalali lakini bila ya
kuwa na vibali halali vinavyoatambulika kisheria, kutokana na maeneo
hayo kutokuwa yamepimwa wala kuwa na ramani ya mipango miji pamoja na
gharama kubwa za urasimihsaji zilizokuwa zinatozwa hapo awali.
"Kiukweli
wananchi wa Kiseriani wamefuhishwa na kuridhishwa na urasimishaji wa
maeneo yao kutokana na kufanyika kwa gharama nafuu tangu zoezi linaze
katika kitongoji changu tuu, cha Losirwai zaidi ya watu 150 wameshalipia
na wengine wanaendelea kulipa na baada ya kulipia tuu, watalamu
wanaweka bicon bila kuchelewa, kupitia zoezi hilo wananchi wamepata
imani kubwa na serikali yao, naweza sema tumepagawa." amesisitiza Katibu
huyo.
Hata
hivyo wananchi hao, wamekiri kupata muamko mkubwa kutokana na elimu
waliyopewa na watalamu pamoja na gharama nafuu za urasimishaji kwa kuwa
kwa muda mrefu wamekuwa wakimilki maeneo yao bila vibali maalumu vya
serikali kutokana na kushindwa kumudu gharama zilizokuwa zinatozwa na
kuongeza kwamba zoezi hilo limekuja wakati muafaka, wakiamaini
litasaidia kuondoa migogoro ya ardhi iliyokuwa inajitokeza kutokana na
udanganyifu uliokuwa unafanywa na watu wasio waaminifu na kwa kuchukulia
kigezo cha uelewa mdogo wa watu wengi.
Rick
Nkya mmiliki wa eneo kitongoji cha Losirwai na Longiva amesema kuwa,
ushirikishwaji uliotolewa na watalamu wa Ardhi, umefanya wananchi kuwa
na uelewa mkubwa juu ya umuhimu wa mipango miji, na kuongeza kuwa kuna
athari kubwa za kuishi kwenye maeneo yasiyopangwa, maeneo ambayo hakuna
miundombinu ya kueleweka huku wananchi wakijenga nyumba zao bila
mpangilio, lakini huku Kiseriani kila mwenye kiwanja amekubali kutoa
mita tano mpaka 6 kwa ajili ya barabara za ndani ya mitaa.
"Binafsi
ninaishi Sakina, wakati nikinunua kiwanja hakukuwa kumepimwa wala
kupangwa, kila mtu amejenga anavyojisikia, jambo ambalo limeasababisha,
ukosefu wa miundo mbinu ya barabara, mpaka sasa kila mtu ana kinjia cha
kufika nyumbani kwake tu na baadhi ya watu hawana kabisha njia, jambo
linalosababisha migogoro mingi miongoni mwa majirani, hata hivyo gharama
zake ni nafuu"amefafanua Nkya.
Naye
Mratibu wa Urasimishaji, halmashauri ya wilaya ya Arusha na afisa
mipango miji, Faiz Mnaro amesema kuwa, tayari wananchi wamepata elimu
ya Urasimishaji, na wamejitokeza kufanya utambuzi na upimaji wa maeneo
yao, pamoja na kukubaliana uwepo wa miundombinu ya barabara katika
maeneo yao, na kuongeza kuwa kutokana na upimaji kila mtaa utakuwa na
barabara za kuanzia Mita 5 - 6, huku barabara za kuunganisha vijiji na
miji zitakuwa na upana wa kuanzia Mita 8 - 15.
Aidha
Mnaro, ameelezea faida za urasimishaji ni pamoja na kuondoa migogoro ya
ardhi, kumiliki ardhi kisheria ukiwa na kumbukubu halali na hatimaye
kupata hati, ardhi inapanda thamani ikiwa imepangwa na kupimwa, inainua
maisha ya watu kwa kuweza kupata mikopo na pia kama dhamana kwa lolote
zaidi shughuli za maendeleo zinafanyika kwa kasi katika maeneo
yaliyopimwa, na kufafanua kuwa urasimishaji ni zoezi kutambua maeneo na
mipaka inafuata kupima, na kupata hati miliki.
Halmashauri
ya wilaya ya Arusha inaendelea na zoezi la urasimishaji katika kijiji
cha Kiseriani katika vitongoji vya Kiseriani, Longiva na Losurwai,
ambapo jumla ya viwanja 3,051 vimetambuliwa na vinatarajiwa kupimwa na
kurasimishwa kwa kuandaa ramani ya Mipango Miji pamoja na wamiliki hao
kupatiwa hati miliki.
No comments :
Post a Comment