Thursday, March 11, 2021

Waliomteka Mchina Arusha wakamatwa Dar es Salaam



Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumteka mtu mmoja raia wa China ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Bonanza ya Jijini Arusha.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 11, 2021, na Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha ACP Justine Masejo, na kusema kuwa watuhumiwa hao walikutwa kwenye moja ya nyumba za kulala wageni maeneo ya ADA Estate Kinondoni Dar es Saalam, wakiwa na mhanga ambaye alikuwa amefungwa kamba.

ACP Masejo, ameongeza kuwa taarifa za utekaji huo walizipata Machi 7 mwaka huu kutoka kwa Lian Qiang, ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Bonanza, na walianza kufuatilia na kubaini kuwa watuhumiwa hao walimsafirisha mhanga hadi Dar es Salaam na kuanza kupiga simu kwa mfanyakazi mwenzake na mhanga wakiomba dola 100,000 ili waweze kumuachia huru

“Baada ya kuwakamata ulifanyika upekuzi ambapo watuhumiwa hao walikutwa na gari aina ya Toyota Kluger mali ya kampuni ya Bonanza lililoibiwa Arusha Februari 8, 2021, lakini pia walikutwa na visu 2, nyundo 1, Drill Machine 1 na Power Cable 5 za Bonanza machine, pamoja na gari lingine aina ya Kluger walilotumia kusafiria kutoka Arusha kwenda Dar es Salaam ambalo lilitelekezwa maeneo ya Clock Tower karibu na eneo la Exim Bank Jijini Dar es Salaam,”  ACP Masejo.

 

No comments :

Post a Comment