Trump alioneoana akipanda ndege aina ya Cessna Citation X, ambayo ni ndogo (super mid-size jet), ndege hiyo ilisajiliwa kwenye kampuni ya Donald Trump mwaka 1997.
Inasemekana ndege hiyo ndogo sana ukilinganisha na wadhifa aliokuwa nao, kwani miezi minne tu iliyopita alikuwa akitumia Air Force One.
Hata hivyo hakuna aliyetegemea kumuona Trump kuendelea kutumia ndege Binafsi (Private 747) baada ya kuondoka Ikulu (White House).
Lakini inashangaza kwà Trump kuonekana akitumia ya Cessna badala ya ndege ya 757 yenye jina lake, inayochukua watu 43 aliyoitumia kipindi cha kampeni.
Hakuna taarifa zinaeleza kwanini ameamua kutumia ndege ya watu 8, ambayo inamlazimu kuinama sana pia hakuna red carpet.
Lakini maisha yanabadilika unavyoishi sio utakavyoishi kesho, unaweza ukapanda au ukashuka.
No comments :
Post a Comment