Mwenyekiti wa kamati wa kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma
na maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo akiongea wakati kikao Mara
baada ya kutembelea mradi wa ujenzi katika taaaisi ya Saratani ya Ocean
Road
Kamati ikiangalia ramani ya ujenzi wa maradi ambao
unatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu mwezi Oktoba na utagharimu
shilingi Bilioni 15.5
Mkurugenzi Mtendaji wa Taaaisi ya Saratani ya Ocean Road
Dkt. Julius Mwaiselage akielezea jinsi mashine ya mionzi inavyofanya
kazi
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Dkt. Dorothy Gwajima akiongea wakati kamati hiyo ilipotembelea hospitali
hiyo
Mmoja wa Wataalamu Kwenye Taaaisi hiyo akiwaelezea kamati
hiyo ramani ya mradi huo itakavyokuwa (Picha zote na Englibeth Kayombo)
**************************************
Na.Catherine Sungura,Dar es Salaam
Serikali imepongezwa kwa
kutenga shilingi bilioni 15.5 kwa ajili ya uwekezaji wa Mradi wa
Ujenzi wa kituo cha Kisasa cha kufanya Vipimo vya Saratani kwa kutumia
teknolojia ya nyuklia (PET CT Scan) pamoja na kiwanda cha kuzalisha
Mionzi dawa (Radio Isotopes).
Pongezi hizo zimetolewa leo na
Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii,
Stanslaus Nyongo, wakati kamati hiyo ilipotembelea Taasisi ya Saratani
Ocean Road (ORCI), iliyopo Dar es Salaam.
Mhe.Nyongo amesema kuwa Serikali
imeipa kipaumbele sekta ya afya, uwekezaji wa mradi huo utakuwa ni wa
kihistoria, wa kimkakati na kwamba utaiweka Tanzania kwenye dira ya
kimataifa kwenye eneo la afya.
Amesema kukamilika kwa ujenzi
huo kutasaidia watanzania na hata wageni kutoka nje ya nchi kupata
matibabu sahihi na kwa wakati ya saratani.
“Hatua hii ni kubwa, mradi huu
itasaidia watu wengi kupata huduma hizi za kibingwa kwa wakati kwani
watu wengi walikuwa wanafika kupata huduma wakiwa Kwenye hatua za
mwisho,” amesema.
Ameongeza kwa kiwanda hiki
wananchi wengi watajua hali zao mapema na uchunguzi utaonesha ugonjwa
umeenea kiasi gani mwilini na Taasisi itakwenda kutambulika mapema zaidi
na kuwatibu na hii ikiwa ni pamoja na magonjwa mengine.
“Ni hatua kubwa watu wengi
watakuja Tanzania kufuata huduma ya vipimo, na Watanzania watanufaika,
watapata tiba sahihi na kwa wakati sahihi, ni jambo kubwa Sana,
mnastahili kupongezwa.
Kuhusu ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mionzi dawa, alisema ni maamuzi sahihi yaliyofanyika kwa wakati sahihi.
“Mmepitia michakato yote, kamati
inawapongeza sana, uwekezaji huu unakwenda kufungua mipaka ya uwekezaji
kwa sekta binafsi vile vile, kwamba mwekezaji yoyote kwa mfano kutoka
India na kwengineko anaweza kuwekeza Tanzania kwa sababu tuna kiwanda
hapa,” alisema.
Alisema uwekezaji huo itakwenda
kuongeza fursa ya utalii wa kimatibabu (medical tourism) kwa Tanzania
kwani watu wengi watapenda kuitembelea.
Kwa upande wa bima ya afya kwa
wote Mhe.Nyongo amesema hatua hiyo ni nzuri kwani itasaidia wananchi
wengi kwakuwa huduma za saratani ni gharama kubwa.
“Niwapongeze Ocean Road kwa
kuendelea kutoa matibabu bure lakini lazima suala la bima kwa wote
tukienda nalo, litamaliza tatizo la changamoto ya gharama kubwa za
matibabu, tutapenda (Wizara) mtuletee mpango huu, tupo tayari
tuhakikishe tupo bega kwa bega, tulichakate pamoja na tulifikishe
bungeni, tuweze kuipitisha,” amesisitiza.
Naye, Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima, amesema Magonjwa
yasiyoambukiza ikiwemo saratani ni tatizo kubwa duniani na matibabu
yake ni ghali Sana.
Amesema Serikali inafanya
Mapinduzi katika kukabiliana na Magonjwa hayo kwani yanachukua watu
wengi(kifo) hata hivyo yanazuilika, ni muhimu jamii kujua namna gani ya
kukabiliana nayo ikiwemo kufanya mazoezi.
“Serikali ni makini hivyo
tunapoelekea Kwenye Bima ya afya kwa wote itasaidia, hata hivyo wizara
inatoa msamaha kwa wagonjwa wote wasio na uwezo ambapo hufuata taratibu
zote za msamaha.
Dkt.Gwajima alitoa wito kwa wananchi kujitokeza kupata uchunguzi wa Afya zao ili waweze kupata matibabu mapema.
No comments :
Post a Comment