Friday, March 12, 2021

RAIS WA ZANZIBAR ALHAJJ DK. MWINYI AMEUFUNGUA MSIKITI WA MASJID TAQWA GOMBANI PEMBA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Mwakilishi wa Mfadhili wa ujenzi wa Masjid Taqwa Gombani ya Kale Pemba.Bw. Humoud Mohammed alipowasili katika viwanja vya Msikiti huo kwa ajili ya ufunguzi uliofanyika leo 12-3-2021. Kabla ya Sala ya Ijumaa.(Picha na Ikulu)

MUFTI Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi akizungumza katika hafla ya Ufunguzi wa Masjid Taqwa Gombani ya Kale kabla kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi kuzungumza na Wananchi na Waumini wa Kiislam katika hafla hiyo.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiondoa kipazia kwa ajili ya ufunguzi wa Masjid Taqwa Gombani ya Kale Pemba akiwa na Mwakilishi wa Mfadhili wa ujenzi huo Bw. Homoud Mohammed,hafla hiyo imefanyika leo 12-3-2021.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na kuagana na Viongozi na Wananchi baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa na ufunguzi wa Msikiti huo wa Masjid Taqwa Gombani ya Kale Pemba.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akiwasalimia na kuzungumza na Waumini wa Kiislam wa Masjid Taqwa Gombani baada ya kumalizika kwa Sala ya Ijumaa na kuufungua rasmis Msikiti huo leo 12-3-2021.(Picha na Ikulu) RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk. Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kwa ajili ya ufunguzi wa Masjid Taqwa Gombani ya Kale Pemba Wilaya ya Chakechake (kulia kwa Rais) Mwakilishi wa Mfadhili wa Ujenzi wa Msikiti huo Bw. Humoud Mohammed na Naibu Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Mahmoud Mussa Wadi.(Picha na Ikulu)

 

No comments :

Post a Comment