Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu ameongoza
maelfu ya wananchi katika Mkoa wa Dar es Salaam kuaga na kutoa heshima
za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt.John Magufuli ambaye
ameagwa leo Machi 20,2021 katika Uwanja wa Uhuru.
Dk.Magufuli
alifariki dunia Machi 17,2021 katika Hospitali ya Mzena Dar es Salaam
ambako alikuwa akipatiwa matibabu ya maradhi ya moyo na leo kwa mujibu
wa ratiba wananchi wa mkoa huo wakiongzwa na Rais Mama Samia wametoa
heshima za mwisho kwa mwanamapinduzi na mpenda maendeleo wa Taifa la
Tanzania.
Kabla
ya Rais Mama Samia kuongoza kutoa heshima za mwisho ilifanyika Misa
maalum katioa Uwanja huo wa Uhuru iliyoanza baada ya mwili kuwasili saa
10:13 asubuhi ukitokea Kanisa la mtakatifu Petro (St.Peters') ambako
nako ilifanyika Misa ya wafu.
Baada
ya Rais Samia kutoa heshima zake kwa Dkt.Magufuli alifuata Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa aiyekuwa amefuatana na mkewe na baada ya Waziri Mkuu
kutoa heshima zake aliondoka uwanjani hapo.Wengine walitoa heshima ni
Mama Maria Nyerere,akifuatiwa na Mama Janeth Magufuli aliyeongozona na
familia yake.
Viongozi
wengine ambao waliotoa heshima za mwisho ni Katibu Mkuu kiongozi Dkt.
Bashiru Ally Kakulwa. Rais mstaafu Aman Abedi Karume, majaji wastaafu
wakiwamo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalaama.Pia viongozi wa ngazi
mbalimbali wakiwemo Mawaziri pamoja na wabunge wa Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.Baada ya hapo wakafuata wananchi waliokuwa
wamesimama katika misururu mirefu.
Awali
wakati akiongoza Misa katika Uwanja huo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar
es Salaam Tadeus Rweich amewaomba watanzania waliojitokeza viwanjani
hapo na waliotazama kupitia televisheni zao majumbani, amumelezea
Hayati Dkt. Magufuli ambapo amesema alikuwa ni Rais aliyeipenda nchi
yake na alifanya kazi zake Kwa uzalendo mkubwa na Kwa nguvu zake zote.
Amesema
Dkt.Magufuli alikuwa ni mtu wa Mungu kweli kwani kila alichokifanya
kwake Mungu alikuwa mbele, alijali maslahi ya Taifa na aliwapenda
Watanzania kwa vitendo.
Aidha
Askofu Rwaich ametoa pole Kwa Rais Mama Samia pamoja na familia ya
Hayati Dkt.Magufuli Mama Janeth Magufuli katika kipindi hiki kigumu
kuwa mstamilivu na kushikamana na Mungu na kubwa zaidi kumuombea.
Pia
ametumia fursa hiyo kutoa pole kwa Watanzania wote na kuwataka kujipa
moyo na matumaini na kwamba yeye hana shaka kwamba Rais Samia atatenda
vyema, haki katika shughuli zake mpya majukumu yake.








No comments :
Post a Comment