Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kiwanda cha Plasco Ltd, Alimiya Osman (kulia) akimwonyesha Waziri wa Maji, Jumaa Aweso mabomba ya kisasa na yenye ubora aina ya Weholite yanayotumika katika miradi mikubwa ya maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Chang'ombe Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso, akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Plasco Ltd inayozalisha mabomba ya Maji wakati alipotembelea kiwanda hicho, jijini Dar es Salaam leo
Waziri wa Maji Juma Aweso,akijaribu kutumia moja ya mashine inayotumika katika utengenezaji wa bomba aina ya Weholite.
Waziri wa Maji Juma Aweso, akimzawadia kiasi cha fedha Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Plasco Ltd inayotengeneza mabomba ya Maji. Edith James baada ya kuridhishwa na maelezo ya kitaalamua kuhusu uzalishaji na mauzo ya mabomba ya kampuni hiyo.
Ofisa Uendeshaji Mkuu wa Kiwanda cha Plasco Ltd, Alimiya Osman,akielezea jambo kwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipotembelea kiwanda hicho kinachozalisha mabomba ya kisasa na yenye ubora aina ya Weholite yanayotumika katika miradi mikubwa ya maji na ujenzi wa miundombinu ya barabara wakati alipotembelea kiwanda hicho kilichopo Chang'ombe Dar es Salaam leo
Kampuni inayotengeneza mabomba ya maji ya Plasco Limted ya Dar es Salaam nchini imetakiwa kusambaza teknolojia yake mpya ya Weholite, inayookoa muda na fedha nyingi za serikali huku pia wakitakiwa kuongeza uzalishaji wa mabomba.
Pia wametakiwa kusambaza mabomba hayo yenye viwango vya
ubora unaotakiwa kwa haraka, kwa sababu kuna miradi zaidi ya 600 ya maji
inayoendelea kutekelezwa katika maeneo mbali mbali nchi nzima.
Hayo
yamesemwa jana na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwenye ofisi za kampuni
hiyo, jijini Dar es Salaam alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea
Makampuni na Viwanda vinavyotengeneza vifaa vya kusambaza majisafi na
majitaka nchini akiambatana na Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo amesema wakandarasi wengi nchini wa miradi ya
maji, wamekuwa wakilia na ukosefu wa mabomba kwamba hayapatikani, wakati
kuna makampuni kadhaa nchini ikiwemo Plasco, yanatengeneza mabomba
mengi na yenye viwango bora.
"Anzisheni miradi ya maonyesho
katika maeneo mbalimbali Onyesheni hiyo teknolojia yenu mpya ya
kutengeneza mabomba ya Weholite hasa katika maadhimisho ya Wiki ya Maji
baadaye mwezi huu..., ikionekana wataalamu wetu wataiona na watasaidia
kuisambaza katika maeneo mengi nchini” amesema Aweso.
Aidha
waziri Aweso ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo makubwa
yanayofanywa na kampuni hiyo ya Plasco na kuongeza kuwa, kuanzia sasa
hataraji kusikia makandarasi wakisingizia ukosefu wa mabomba, kwamba
ndiyo yanawakwamisha kukamilisha miradi, kwa sababu katika ziara yake
leo jijini Dar es Salaam, amebaini kuwa mabomba yanapatikana kwa wingi.
Amesema
kama kuna mkandarasi ataendelea kusingizia ukosefu wa mabomba, basi
aondolewe katika miradi, badala yake wizara itatumia wataalamu wake
ambapo kwa kutumia wataalamu wake, wizara imeokoa fedha nyingi na
kuiwezesha kwa muda mfupi kutekeleza miradi 192 iliyokwama.
Ameongeza
kuwa, miradi hiyo kama ingeendelea kutekelezwa na makandarasi waliojaa
visingizio visivyokwisha, ingegarimu Sh. bilioni 207 lakini kwa kutumia
wataalamu wake Wizara imetumia Sh bilioni 193 na kuwawezesha kuokoa
mabilioni ya fedha za serikali.
Wateja wakubwa wa Kampuni ya
Plasco ni Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) na mamlaka za majisafi na
usafi wa mazingira za miji mbalimbali nchini. Asilimia 80 ya wateja wa
Plasco ni serikali na taasisi zake.
KWa upande wake Afisa
Uendeshaji wa Kiwanda cha Plasco, Alimiya Osman amesema wanafurahi
kutembelewa na Waziri wa Maji Jumaa Aweso na Uongozi mzima wa RUWASA na
DAWASA na kuahidi kuendelea kushiriana kwa ukaribu zaidi na wizara hiyo
ili kuongeza ufanisi katika kazi zao.
Amesema kwa sasa wanazalisha malighafi za tani 28,000 kwa mwaka ambapo katika tani hizo asilimia 70 ni mabomba ya plastiki.







No comments :
Post a Comment