Sunday, March 28, 2021

MZEE MWINYI, KIKWETE WATOA YA MOYONI KUHUSU DK.MAGUFULI...WASIMULIA JINSI WALIVYOMPENDA, KUMUAMINI NA KUMTUMAINIA




Said Mwishehe ,Michuzi TV-

RAIS Mstaafu Mzee Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu Jakaya Kikwete wamemzungumzia aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu ya

Tano Hayati Dk.John Magufuli huku wakieleza kifo chake kimewaumiza sana wao na Watanzania wote.

Wakizungumza leo wakati wa kitoa salamu baada ya kufanya Ibada Maalum ya kumuombea Dk.Magufuli kwa Mungu ampe pumziko la milele na apushwe na adhabu za kaburini.

Mzee Mwinyi akizungumza mbele ya waombelezaji hao wakiongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan , amesema msiba huo ni mzito kwa watanzania wote "Natoa pole kwa Rais Mama Samia,natoa pole kwa mama Janeth Magufuli, pamoja na watoto wetu, sio peke yako nasema poleni.Nawapa pole Mheshima Hussein Mwinyi pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

"Nilimpenda sana Dk.Magufuli,kifo chake kimemshutua sana,baada ya kupata taarifa ya kifo nilikaa kimya kwa dakika mbili nikitafakari.Jambo ambalo ametuachia,pale alipofanya kijana huyu, kutekeleza maagizo ya baba wetu wa Taifa mzee Nyerere,kijana huyu amewaza na kuamua tuhamie Dodoma,na kutekeleza jambo hilo kwa miaka miwili.

 " Sisi wengine tulichukua miaka 40 na hatufanya hivyo.Sio hilo tu ndugu yetu Dk.Magufuli amefanya mambo mengi sana na makubwa,mazuri na ya maana, ameyatekeleza kwa niaba yake na kwa niaba ya sisi wengine  ambao hatukuwahi kutekeleza.Watanzania wenzangu, kwa kipindi cha miaka mitano tumepiga hatua,Dk.Magufuli ameishangaza dunia.

"Ameleta maendeleo makubwa.Dk.Magufuli ameunganisha nchi kwa barabara za lami kwa muda mfupi wa miaka mitano, alikuwa mzuri wa  takwimu angetuambia, lakini niseme barabara nyingi zimejengwa kwa muda mufupi.Amerahisha biashara na masoko kwa kutokana na  uhakika wa mawasiliano,  ndege zimerudi nchini, madege yetu wenyewe yanayokwenda kila mahali,"amesema Mzee.Mwinyi.

Ameongeza ndio maana leo wako hap."Mama Siti yuko mbali ningemuuliza panaitwaje hapa, Chato.Huyu kijana wetu Hayati Dk.Magufuli  amewaondolea fedheha Wamachinga ya kuwindwa kando kando za barabara, kwanza aliwapa muda rudini huko huko huko barabarani,na kuahidi kuboresha mazingira ya biashara, anahurumia wanyonge, amewainua.

"Wamachinga amewaondolea manyanyaso ya kuwindwa kama ndege watundu, badala yake aliahidi kuwatengeneza mahala bora zaidi, sio machinga tu hata akina sie tumeingia kwenye huruma hiyo.Walikuwa wamepata mtu wa kuwasemea, wa kuwafanya waonekane wa maana , huyu ndio Magufuli.

"Msinichoke kunisiliza na Watanzania wenzangu,aliyekuwa Rais wetu John Magufuli alifanya kazi kubwa, ya kuinua wazee na masikini, narudia kwa kipindi kifupi cha miaka mitano nchi yetu ilipiga hatua kiasi cha kushangaza ulimwengu, kwanini? 

" Alikuwa si mtu wa maneno alikuwa wa vitendo na mfuatiliaji.Rais Magufuli amefanya mengi na kuondoka kwake ni msiba kwa kila mmoja wetu.Kama nilivyosema amefanya mengi, kila mmoja afikirie.

Kuhusu Rais Samia Suluhu Hassan , Mzee Mwinyi amesema kuwa" Mama Samia ,Dk.Magufuli ameondoka,ametuachia wewe uliyekuwa msaidizi wake wa karibu sana ,alichokusudia ndicho ambacho umekusudia wewe. Nimefurahi sana kusikia ile kauli kwamba wewe ndio Rais,kwa hiyo niseme, mambo mawili,upokee pole kwa kuondokea na mpendwa wetu Hayati Dk.Magufuli na upokee pongezi kwa kupanda cheo,sote tunakuombea dua,mambo yaende vizuri, nchi hii uiweze,na ushaiweza. "

Awali akitoa salamu kwa waombolezaji, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ametumia wake mwingi kumueleze Hayati Dk.Magufuli na jinsi.ambavyo alivyoipenda nchi yetu ya Tanzania,amemuelezea jinsi alivyokuwa mchapakazi na ameeleza alivyopanga naye mikakati ya kumsaidia katika ujenzi wa barabara nchini huku akielezea alivyomuamini na kumtumaini tangu akiwa Waziri.

Ametumia nafasi hiyo kuelezea namna ambavyo alimpenda Dk.John Magufuli kutokana na uchapakazi wake na huwa anashangaa anaposikia baadhi ya watu wakisema hampendi Dk.Magufuli.Katika kuthibitisha jinsi alivyompenda na kukumbali, Kikwete amesema katika uongozi lazima uache alama,hivyo katika utawala wake alimtumia Dk.Magufuli.kuacha alama ya barabara nchini, na walifanikiwa.

"Ngoja niwaambie niliamua kumuita Dk.Magufuli na kumwambia atakuwa Waziri aa Ujenzi na tukawa na makubaliano sitamhamisha, kikubwa ilikuwa ni kumuwezesha ili atekeleze.majibu yake,wote ni mashahidi kwa kazi ambayo jembe langu JPM aliifanya.

"Hata wakati naelekea kustaafu jina lake nilikuwa nalo.muda wote katika watu watano ambao nilitaka mmoja wapo awe Rais baada ya mimi, nilijenga hoja kwanini.Magufuli, pamoja na mivutano.mimi nilijenga hoja tu na hatimaye akawa Rais wetu,nimeona leo niseme hili watu waelewe.

Aidha, Mzee Kikwete amesema kwamba hatasoma tena SMS  za Dk.Magufuli alizokuwa anawasaliana naye saa nane usiku."Ukiona simu ujue yeye, siku moja nikamwambia hulalia? Akanijibu nimejifunza kwako. Nafarijika sana ,ameacha alama ambazo zitadumu kwa kizazi cha sasa na kijacho, amegusa maisha ya wengi.

"Amepata bahati ya kusifa akiwa hai,amepata bahati ya kuliliwa na kupendwa,tumeshuhudia umati wa watu kila mahali.Wana CCM  tujiepushe kuimba nyimbo za adui zetu,tutafarakana na kugawanyika, naogopa kuendelea kumuelezea tusije kukufuru.

Ameweka wazi katika utawala wake,alimuamini sana Dk.Magufuli,alimtumainia na kwamba hata alipoona kwenye Wizara kuna changamoto aliamua kumpeleka Dk.Magufuli na aliondoa changamoto,hivyo alikuwa muhimu sana ya yeye kufanikisha yale ambayo aliahidi kuona yanatekelezwa kwa ajili ya Watanzania.

Akimzungumzia ,Rais Samia Suluhu Hassan, Kilwete amesema kwa waliostaafu wao wanamuda mwingi na wa kutosha maoni ya mitandaoni."Umetuhakikishia  kuwa nchi iko katika mikono salama,hakuna kitakachoharibika.Baada ya matatizo ya Zanzibar,Rais Mkapa aliunda Tume niliyoongoza mimi, lakini nilikufahamu zaidi Mama Samia ulipokuwa Waziri wangu katika Wizara ya Muungano.

"Ulifanya vizuri sana,sina shaka muungano wetu utaendelea kudumu, hata hivyo kipaji chako cha uongozi kilionekana na kuchanua ulipokuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba na hapo ndipo tukaona unatosha kuwa kiongozi mkubwa, ndio maana mwaka 2015 tutakuchagua kuwa mgombea mwenza,ukashiriki kuomba kura na tukashinda, na mwaka 2020 katika Uchaguzi Mkuu umefanya tena hivyo.

"Matarajio ya watanzania unayajua, wewe sio mwanagenzi bali umepikwa umepikika, wewe ni mtu sahihi,tunaimani kubwa na wewe,ni mchapakazi.Mimi na wastaafu wenzangu tutakuwa pamoja nawe, uliomba tushirikiane, ukitutuma tutakuitika.Ukituita tutaitika,ukikaa kimya na sisi tutaendelea na mambo yetu.

 

No comments :

Post a Comment