Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuwaongoza watanzania katika ibada maalum ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli, Shughuli za kuaga mwili zitafanyika kuanzia leo mpaka kesho ambapo viongozi mbalimbali watashiriki kuaga pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam.
(PICHA NA JOHN BUKUKU -DAR ES SALAAM)
Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakiwa tayari kupokea mwili wa Hayati Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Uhuru.
Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye gari maalum la kijeshi kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ibada maalum na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuaga.
Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ukiwasili kwenye uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ibada maalum na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuaga.
Viongozi mbalimbali wakiingia kwenye uwanja wa Uhuru wakati wmili wa Hayati Dk. John Pombe Magufuli ulipowasili kwa ajili ya ibada.
Mwili wa Aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dk. John Pombe Magufuli ukitolewa kwenye kanisa la Saint Peter Oysterbay kuelekea uwanja wa Uhuru kwa ajili ya ibada maalum na viongozi pamoja na wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kuaga.
Baadhi ya wasaidizi wa hayati Dk. John Pombe Magufuli wakiingia kwenye uwanja wa uhuru kwa ajili ya kushiriki ibada hiyo.
Picha mbalimbali zikionesha hali ya simanzi na majozi ilivyokuwa wakati mwili wa hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli akipita katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kwenda uwanja wa Uhuru ambako ibada maalum ya kuaga mwili inafanyika.
No comments :
Post a Comment