Wednesday, March 31, 2021

Mabadiliko ya baraza la mawaziri Tanzania

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.

Mabadiliko hayo ameyafanya hii leo katika Ikulu ya Chamwino Jijini Dodoma wakati wa hafla ya kumuapisha makamu mpya wa Rais wa nchi hiyo. Mwandishi wetu.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa ameamua kufanya mabadiliko ili kuweka mambo sawa hasa wakati huu wa bunge la bajeti linaloendelea Jijini Dodoma.

Kulingana na Rais Samia, aliyekuwa waziri wa katiba na sheria Mwigulu Nchemba sasa ndio waziri mpya wa Fedha, ambapo amechukua nafasi ya Makamu wa Rais Dkt Philip Mpango.

Liberata Mulamula waziri mpya wa wizara ya mambo ya nje wa Tanzania.

Aussenminister Palamagamba Kabudi von Tansania

Waziri mpya wa Katiba na Sheria Palamagamba Kabudi

Liberata Mulamula ndiye waziri mpya wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki. Kabla ya uteuzi wake, Mulamula alikuwa katibu mkuu wizara ya mambo ya nje. Aidha amewahi kuhudumu kama balozi katika nchi mbalimbali. Palamagamba Kabudi ameteuliwa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Kabudi alikuwa anashikilia wadhifa wa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Ummy Mwalimu ameteuliwa kuwa waziri katika Ofisi ya Rais Tamisemi akibadilishana na Selemani Jafo ambaye ameteuliwa kuwa waziri ofisi ya Makamu wa Rais ofisi ya zamani ya bi Ummy Mwalimu.

Wizara ya Uwekezaji ambayo awali ilikuwa chini ya ofisi ya Rais sasa imepelekwa chini ya ofisi ya Waziri mkuu, ambapo Waziri katika Wizara hiyo ni Godfrey Mwambe. Daktari Bashiru Ally ameteuliwa kuwa mbunge na mahala pake kuchukuliwa na balozi Hussen Yahya Katanga ambaye ndiye sasa Katibu Mkuu kiongozi.

Mawaziri walioteuliwa watakula kiapo hapo kesho (01.04.2021) katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma Tanzania.

Chanzo: DW dodoma

 

No comments :

Post a Comment