Thursday, March 18, 2021

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA YAKAGUA MIRADI YA NSSF

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Najma Giga, akizungumza wakati wa kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Dar es Salaam.
Waziri wa nchi, ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, ambaye pia ni Mbunge, akizungumza wakati wa kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),  Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa  Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF), Ndg. William Erio, akitoa semina kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, katika Ofisi za Bunge jijini Dar es Salaam, kabla ya kuelekea kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Mfuko huo.

Meneja miradi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Ndg. Helmes Pantaleo, akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Kamati hiyo  imekagua miradi mbalimbali iliyo chini ya NSSF, iliyopo jijini Dar es Salaam.
 
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii  (NSSF),  jijini Dar es salaam.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, ikikagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini yaMfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF),  jijini Dar es salaam.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, imekagua miradi mbalimbali iliyo chini ya Shirika la Taifa la mfuko wa hifadhi ya jamii (NSSF), hapa kwenye majengo mawili ya Mzizima Tower, Posta Mpya jijini Dar es salaam.
***************************


Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, ikiongozwa na Makamu Mwenyekiti, Mhe. Najma Giga na Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu  Mhe. Jenista Mhagama,  imetembelea na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyo chini ya Mfuko wa  Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

 Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), lipo chini ya Wizara ya nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mujibu wa sheria, huku Mhe. Jenista Mhagama akiwa ni Waziri mwenye dhamana kwa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Miradi iliyokaguliwa leo ni miradi ya hoteli, apartments na nyumba za kawaida za kupanga zilizopo Dar es salaam.

Miradi hiyo ni Mzizima Tower, majengo mawili yaliyopo Posta mpya,
 jijini Dar es Salaam, yenye hoteli ya vyumba 90, apartments 44, eneo kwà ajili ya ofisi, yenye eneo la mraba 8502, maegesho ya magari 354, mradi ukitegemea kugharimu bilioni 220 na mpaka sasa ukiwa umegharimu shilingi bilioni 125. Mradi umekamilika kwa 85%, ukitarajiwa kukamilika Juni mwaka huu.

Mradi mingine ni ile ya apartments na nyumba za kawaida za kupanga zilizopo Toangoma, gharama yake ikiwa ni shilingi bilioni 161 mpaka sasa zikiwa zimetumika shilingi bilioni 61.

 Dungu Kigamboni ni nyumba 100, huku nyumba 94 zikiwa zimekamilika na kati ya hizo nyumba 25 zikitumiwa na viongozi mbalimbali, wafanyakazi wa Manispaa ya Kigamboni na wananchi wengine.

 Mradi wa Mtoni Kijichi Dar es salaam ni mradi wa nyumba 292 katika awamu ya kwanza (1),  zikitegemewa kujengwa nyumba 820 katika awamu tatu (3), mradi ukikamilika utagharimu shilingi bilioni 159 na hadi sasa mradi umegharimu shilingi bilioni 125.5.

Mradi wa Dungu Kigamboni, umegharimu shilingi bilioni 64 ukiwa ni mradi wa nyumba 134.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Najma Giga, amesema, miradi hii ni mikubwa na ina manufaa  kwa uchumi wa Taifa na tija kwa maisha ya Watanzania waliopo katika uchumi wa kati, akiwataka NSSF kutumia mbinu mbalimbali kuhakikisha miradi hii inaleta tija kwa Taifa.

Naye Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye naye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mhe. Jenista  Mhagama, akiongea kwa niaba ya Serikali ameitaka Kamati hiyo kuishauri Serikali vizuri, huku akisisitiza kuwa NSSF kupewa kushughulika na sekta binafsi.

Amesema "NSSF ikijipanga zaidi Shirika linaweza kufanya vizuri, Serikali imeingilia kati kwa mradi wa Mtoni Kijichi, ikitaka mradi uanze kufanya kazi, huku nyumba hizo zikianza kutumika kama hostels za vyuo mbalimbali hapa Dar es Salaam"

Akizungumza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)  Ndg. William Erio, ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa ushauri mbalimbali, huku akisema baada ya miradi ya nyumba, sasa Mfuko tayari una ajenda ya kuwekeza katika sekta ya viwanda, ili kuhakikisha unatoa ajira kwa Watanzania walio wengi, kwa sasa tayari wameanza na kiwanda cha sukari.

 

No comments :

Post a Comment