Monday, March 15, 2021

KAMATI YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI (PAC) YAKAGUA MRADI WA UZALISHAJI SUKARI ENEO LA MBIGIRI MKOANI MOROGORO LEO MACHI 15, 2021.


Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiwasili katika Ofisi za Mkulazi Holding  Company kukagua mradi wa shamba la uzalishaji Sukari eneo la Mbigiri (Dakawa) Morogoro leo Machi 15, 2021.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama akifafanua jambo mbele  ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) walipotembelea na kukagua mradi wa uzalishaji Sukari wa Mkulazi Holding  Company eneo la Mbigiri (Dakawa) Morogoro leo Machi 15, 2021. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Naghenjwa Kaboyoka na Kulia ni Makamu Mweyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Japhet Hasunga.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Mhe. Naghenjwa Kaboyoka (katikati) akizungumza wakati Kamati hiyo ilipotembelea na kukagua mradi wa uzalishaji Sukari wa Mkulazi Holding  Company eneo la Mbigiri (Dakawa) Morogoro leo Machi 15, 2021.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) wakiongozwa na  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama  (mwenye mwavuli) wakikagua mradi wa shamba la uzalishaji Sukari wa Mkulazi Holding  Company eneo la Mbigiri (Dakawa) Morogoro leo Machi 15, 2021.

PICHA NA BUNGE

 

No comments :

Post a Comment