
JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya limefanikiwa kuwakamata raia wa Burundi 05 wakiwa na watoto wao 05 kwa kosa la kuingia nchini bila kufuata taratibu za nchi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya SACP Ulrich O. Matei imeeleza kwamba tarehe 10.02.2021 majira ya saa 12:30 mchana huko kijiji na kata ya Changalawe, Tarafa Kiwanja, wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya . Askari Polisi wakiwa doria walisimamisha Basi la abiria yenye namba T.353 ANS inayomilikiwa na Kampuni AN ikitokea Mkoa Tabora kwenda Mbeya.
Askari walianza kufanya ukaguzi kwenye basi hilo na ndipo walimkamata NDAYIPEUKAMIYE SADOCK [37] Raia na Mkazi wa nchini Burundi akiwa na wenzake 04 pamoja na watoto wao 05 kwa kosa la kuingia nchini bila kibali. Taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.

No comments :
Post a Comment