Monday, February 8, 2021

SERIKALI YAOMBWA KUTOA ELIMU KWA WAKULIMA JUU YA AFYA YA UDONGO

…………………………………………………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.
Kampuni inayojishughulisha na upimaji wa udongo kwa wakulima wakubwa,wakati na wadogo(LSSL)imeiomba serikali kupitia maafisa ugani kutoa elimu kwa wakulima juu ya umuhimu wa afya ya udongo.
Akiongea na waandishi was habari  mkurugenzi wa kampuni hiyo Dkt Edmond Matafu alisema kuwa bado wakulima wengi hawana ulewa juu ya afya ya udongo ambayo ndio msingi mkubwa wa kilimo.
Alisema elimu bado haijawafikia wakulima walio wengi hali inayopelekea kutokuona umuhimu wa kupima udongo  na kuendelea kulima kilimo cha mazoea kisichokiwa na tija.
Dkt Matafu alieleza kuwa Kuna faida kubwa za kupima udongo moja wapo ikiwa ni kujua aina ya mazao yanayofaa katika shamba la mkulima, kujua virutubishi vilivyopo katika udongo na ni kwa kiasi gani, pamoja na mkulima kununua mbole kulingana na upungufu wa virutubishi vinavyohitajika kwenye udongo.
“Hii itasaidia kupunguza gharama kwani wakulima wamekuwa wakitumia mbolea hata kwa mashamba ambayo yana virutubisho vya kutosha na wakati mwingine kutumia mbolea isiyofaa kwa eneo husika jambo linaloongeza gharama na kuleta hasara kwa kutokupata  mazao ya mimea aliyootesha,”Alisema Dr Matafu.
Alifafanua kuwa  faida nyingine ni kusaidia kutunza mazingira kwasababu baadhi ya virutubishi vikizidi kwenye udongo huweza kuharibu mazingira na kufanya mimea ya aina yoyote isiweze kuota ambapo mkulima atakapo pima udongo katika shamba lake atajua mahitaji ya mbolea au virutubishi vinavyohitajika na kujua jinsi ya kuboresha udongo huo.
Alieleza kuwa lengo la kuhamasisha upimaji wa udongo ni ili kuwasaidia wakulima wote nchini kujua afya ya udongo hasa tindikali (PH), kujua virutubishi vilivupo katika udongo kabla ya kulima zao lolote na kuwezesha kujua kias i cha mbolea inayojitajika katika mmea.
“Kwa kupima udongo mkulima atajua virutubishi vilivyoko kwenye udongo Kama vile Organic, Carbon, Nitrogen, Sodium, potassium pamoja na virutubisho vidogo vidogo ambavyo ni muhimu kwa ukuaji na uzalishaji wa mmea Kama vile boron, zinc, copper, Cobalt, silicon na kuendelea,” Alieleza.
Alifafanua kuwa ni muhimu kwa wakulima kabla ya kulima au kuotesha kujua kujua afya ya udongo wa shamba lake ili kuweza kufanya kilimo chenye tija ambapo anatakiwa kuchukua sampuli ya udongo kwa njia ya kupshanisha (zigzag)na kupeleka katika maabara ili kujua aina ya mbolea na mazao yanayokubali katika eneo hilo.
“Majibu mazuri ya udongo yanatokana na umakini wa uchukuaji wa sampuli katika shamba ambapo anayechukua udongo anatakiwa kuchima vishimo zaidi ya 15 vyenye kina Kati ya sentimita 15 hadi 20 na kukusanya sapuli hizo toka maeneo mbalimbali ya shama analotarajia kulima,”alifafanua.
Aliendelea kusema kuwa baada ya kukamilika kwa zoezi la ukusanyaji wa sampuli, udongo huo utapelekwa katika maabara ambapo majibu yake yatatoka baada ya siku kaadhaa lakini pia kina kifaa cha kupima udongo papo kwa hapo.
“LSSL tuna aina mbili za teknolojia za kupima udongo moja ya papo kwa hapo na nyingine ni ya maabara ambapo hii ndio inayotoa majibu mengi zaidi ikiwa ambayo Ni pamoja na aina ya mazao yanayofaa katika shamba lakini Kuna maeneo mengine pia majibu yanatoka kuwa hapafai kulima zao lolote na hapa panahitajika jitihada za kurutubisha udongo,” Alisema
“Kuna madhara unapoweka mbolea mahalo pasipo hitaji mojawapo ikiwa ni kuharibu udongo na kupunguza uzalishaji wa mazao na sisi LSSL tunapima udongo ili kusaidia wakulima kuongeza tija ya mazao wanayozalisha,”alibainisha.
Kwa upande wake Alen Andrew meneja masoko wa kampuni hiyo alisema kuwa kampuni hiyo inafanya kazi nchi mzima ambapo asilimia kubwa ya wakulima waliojitokeza kupima udongo wao ni kutoka nyanda za juu kusini na katika meneo mengine mwamko bado ni mdogo.
“Hii ni huduma mpya wengi bado hawana uelewa ww umuhimu wa kupima udongo lakini nisisitize kuwa kutumia mbegu Bora na mbolea bila kufahamu afya ya udongo hakiwezi kuleta tija,”Alieleza Alen.
Alieleza ikumbukwe kuwa udongo ndio msingi wa kilimo hivyo wakulima wawekeze kwenye afya ya udongo ili waweze kulima kilimo Bora chenye manufaa kwao na kwa taifa zima.
Alisema teknolojia waliyonayo inauwezo wa kupima udongo kwa haraka zaidi bila kuhitaji kenikali ambapo kwa siku wanaweza kupima sampuli zaidi ya 50.

 

No comments :

Post a Comment