Mfanyabiashara wa maziwa Lopeny Tajiri akiwaeleza waandishi wa habari jinsi taasisi ya mfuko self ilivyomsaidia
Na Woinde Shizza , Michuzi Tv -ARUSHA.
Tasisi
ya serikali iliyopo chini ya wizara ya fedha ya Mfuko Self
unaojihusisha na utoaji wa mikopo ya biashara, kilimo pamoja na mkopo
wa haraka wa wajasiriamali umetoa mkopo wa billion 215 kwa wanufaika
zaidi ya 100,000.
Akizungumza na Wandishi wa habari Mkurugenzi wa maendeleo ya biashara wa mfuko
huo Mary Kipeja katika maonesho ya nne ya mifuko ya programu za
uwezeshwaji wanawake kiuchumi yanayoendelea jijini Arusha, alisema kuwa mpaka
sasa wamewafikia wananchi 158,000 ambapo wana matarajio ya
kuwafikia wananchi wengi zaidi.
Bi
Kipeja alisema wataweza kuwafikia wananchi wote kwani watafungua
matawi mikoa yote nchini ambapo kwa sasa wapo Dar es salaam, Mbeya,
Arusha, Mwanza, Zanzibar, Shinyanga pamoja na Dodoma.
Alieleza
mfuko huo mbali na kutoa mikopo wanatoa elimu kwa wateja wao ili waweze
kufikia malengo yao baada ya kuchukua mkopo wakaelekeze walipokusudia
na sio kwenda kufanyia mambo mengine yatakayyowafanya washindwe kulipa.
Alifafanua
kuwa lengo la mfuko huo ni kukuza na kuboresha upatikanaji wa huduma za
kifedha kwa wananchi hasa wa vijijini kwa kuwapa fursa ya kushiriki
katika shughuli za uzalishaji mali.
“Tunataka
wananchi wajiongezee kipato na kuondokana na umasikini ambapo tunatoa
mikopo ya jumla na mikopo ya kwaajili ya mtu mmoja mmoja hivyo na
wakaribisha watanzania wrote wenye uhitaji kuja Self na kuondokana na
changamoto ya ukosefu wa mitaji,” Alisema mkurugenzi huyo.
Mmoja
wa wajasiriamali aliyenufaika na mkopo kutoka katika mfuko huo Lupen
Tajiri ambaye ni msindikaji wa maziwa kutoka Kata ya Olturumet
iliyopo wilayani Arumeru mkoani Arusha, alisema kuwa
alishazunguka katika tasisi nyingi za fedha lakini hakupata mafanikio
kutokana na kuonekana kuwa hakopesheki lakini mfuko huo ulimsaidia.
“Waliona
andiko langu litaenda kuwasaidia wananchi wa chini ambao ndio ninanunua
maziwa kutoka kwao na kuyasindika kwa muda wa mwaka mmoja sasa na
ninanunua kwa watu wa kawaida kabisa,” Alisema Lupen Tajiri.
Alieleza
mfuko huo umemsaidia kutimiza malengo yake ya kuendeleza sekta ya
maziwa ambapo awali hali nilikuwa ngumu kwani mabenki waliona kumkopesha
ni kuingiza taasisi mashakani.
No comments :
Post a Comment