*Wadaiwa kuomba sh.milioni 100 baada ya majadiliano wachukua sh.milioni 20 kwenye moja ya benki ya NMB
*Watumishi hao wadaiwa kufanya unyanyasaji kwa wamiliki wa kiwanda
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
NAIBU Waziri wa Viwanda na Biashara Exaud Kigahe ameliagiza Shirika la
la Viwango Tanzania (TBS) kuwasimamisha kazi wafanyakazi wa watatu waliokwenda kufanya ukaguzi usiofuata hilo taratibu za shirika hilo huku huku uchunguzi ukifuata dhidi yao.Wafanyakazi hao ni Afisa Viwango Suleiman Banza, Dereva Issa Mbaruok Dodo pamoja na Afisa Usafirishaji Thomas Mwamkinga wote hao wanadaiwa kwenda katika kiwanda cha smart Industry Limited ambapo Suleiman Banza alidai wanafanya ukaguzi huo pamoja na polisi wakidai kuwa kiwanda hicho wanatumia bidhaa zilizoisha muda wake.
Kagahe amesema waliweza kumbana mwenye kiwanda na kutaka kuwapa sh.milioni 100 ambapo waliweza kujadiliana kutoka sh.100 wakaja sh.milioni 50 ikashindikana wakafikia sh.milioni 20 ambayo haikuwepo katika mazingira ya kiwanda na kisha kwenda benki ya NMB wakachukua na kilichofuata waliwanyang'anya simu na kuwaweka chini ulinzi wenye kiwanda.
Naibu Waziri Kagahe amesema Suleiman Banza alijitambulisha kwa mwenye kiwanda kuwa yeye ni Afisa Ukaguzi wakati nafasi yake ni Afisa Kiwango, Dereva kosa lake ni kwenda kumpeleka Afisa huyo kwenye kazi haramu na Afisa usafirishaji kosa lake ni kutoa gari ya kumpeleka aliyejifanya mkaguzi.
Amesema kuwa wakati serikali ikiwa inahamasisha uwekezaji katika sekta binafsi yenye kuajiri watanzania wengi wapo baadhi ya wafanyakazi wasiowaadilifu wanakwamisha za juhudi za serikali ya awamu ya tano.
Naibu Waziri huyo ametaka TBS kushirikiana na vyombo vingine ikiwemo Taasisi ya Kupambana na rushwa(TAKUKURU,) pamoja na polisi ambao walikwenda katika operesheni hiyo haramu ya kufanya unyanganyi na udhalilishaji kwa mmiliki wa viwanda.
Hata hivyo Naibu Waziri amewataka wafanyakazi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuwa na maadili katika utumishi wao na kuongeza kuwa baada ya uchunguzi huo tararibu zingine zitafuata ikiwemo na mahakamani.
No comments :
Post a Comment