Sunday, February 7, 2021

NDEGE INSURANCE WALIPONGEZA SHIRIKA LA BIMA LA TAIFA (NIC) KWA KUZINDUA BIDHAA MPYA INAYOWAJALI WATEJA WAKE


Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers Dkt. Sebastian Ndege akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dar,mara baada ya Shirika la bima la Taifa (NIC,) kuzindua bidhaa yake  kubwa na maalum iitwayo 'Bima Flex'
Sehemu ya uongozi wa Shirika la bima la Taifa (NIC,) na wadau wao wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo ukumbini humo leo jijini Dar
Pichani kushoto ni Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers Dkt. Sebastian Ndege na Wadau wengine wakiafuatilia tukio la uzinduzi huo wa bidhaa mpya ya Shirika la bima la Taifa (NIC,)iitwayo 'Bima Flex'.
 
 =========  ==============  ==============

 NDEGE Insurance Brokers ambao ni wawakilishi, wataalamu na madalali wa bima nchini, 

wamelipongeza  Shirika la bima la Taifa (NIC,)  kwa kuzindua bidhaa maalumu ya 'Bima Flex' kwa ajili ya kutoa huduma za bima kwa kuzingatia unafuu katika ulipaji ili kuepuka changamoto za malipo kwa Watanzania na kuleta maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Ndege Insurance Brokers Dkt. Sebastian Ndege amesema kuanzishwa kwa "Bima Flex" ni mkakati wa kutoa unafuu kwa watanzania hasa wa kipato cha chini na wanaopenda maendeleo katika kulinda mali zao zikiwemo nyumba na magari.

"Bima Flex imejikita zaidi katika bima ya magari ambayo kwanza  inatoa unafuu katika ulipaji kwa kulipa kwa awamu, pili ni kukulipa ndani ya siku saba pale ajali inapotokea pamoja na kutochangia kiwango chochote kwa mali iliyopata ajali." Amesema.

Amesema, Bima Flex inatoa nafasi ya kulipa kwa awamu na kupata mafao pindi linapotokea tatizo katika vioo vya magari bila gharama za ziada.

Vilevile ameeleza kuwa "Bima Flex inasimamia  sera yake ya unafuu na kutoa huduma kwa haraka zaidi na kwa kuzingatia ulipaji wa awamu bila riba au makato yoyote ya awali au baada, utakachokopa ndicho utakacholipa."

Ndege amewashauri watanzania kutumia bima ya Taifa kwa manufaa ya taifa na hiyo kwa kutembelea Ndege Insurance Brokers katika Ofisi zilizopo Azikiwe jijini Dar es Salaam na Posta jijini Mwanza kwa ushauri na kupata huduma kwa haraka zaidi.

Aidha amesema kuwa, Shirika la bima la Taifa (NIC,) ni la kizalendo linalohudumia watanzania na soko la watanzania na ushirikiano huo wa kuleta maendeleo kwa Taifa na umma wa watanzania.

 

No comments :

Post a Comment