Wednesday, February 10, 2021

NAIBU WAZIRI KATAMBI AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI WCF

NA MWANDISHI WETU, MOROGORO

NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Patrobas
Katambi amezindua Baraza la Wafanyakazi Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) na


kutoa wito kwa wafanyakazi kuchapa kazi kwa bidii kwani ndio nguzo kuu katika
mafanikio ya Mfuko.

Mhe.
Katambi ameyasema hayo mjini Morogoro leo Februari 10, 2021 wakati akizindua
baraza la Wafanyakazi WCF kwenye ukumbi wa Magadu.

“Lazima
tujue uwajibikaji ni nguzo kuu ya mafanikio katika sehemu yoyote ya kazi, hivyo
wajumbe mnaowawakilisha wafanyakazi wa Mfuko mnapaswa kuwahimiza wenzenu kuhusu
 swala hilo.” Alifafanua  Mhe. Katambi.

Alisema
Serikali inatambua mchango wa wafanyakazi wote nchini lakini vile vile inatambua
sana  na kuheshimu mchango wa Mfuko wa
Fidia kwa Wafanyakazi katika kukuza uchumi wa nchi yetu kwa kuhakikisha kuwa nguvu
kazi ya wafanyakazi wanaougua au kuumia kutokana na kazi haipotei kwa wakati
wote kupitia huduma ya matibabu inayotolewa kwa waathirika.

“Napenda
niwahakikishie kuwa Serikali ya awamu ya tano inaendelea kushirikiana na Mfuko
katika kuhakikisha unanufaisha watu walio wengi na kufanikisha malengo ya
kuanzishwa kwake.”

Naibu
Waziri Katambi pia aliupongeza Mfuko huo kwakuwa na wafanyakazi wachache lakini
waliouwezesha Mfuko kupiga hatua kubwa katika utekelzaji wa majukumu yake.

“Mnatupa
heshima kubwa sana ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Waziri mama Jenista Mhagama
tangu mmeanza kutekeleza majukumu haya mmeanzia ziro baada ya mwaka mmoja
mkalipa shilingi bilioni 1.5 habari
hizi zinafurahisha hata kamati ya bunge ilishukuru na kuwapongeza hongereni sana
sana.” Alisema Mhe. Naibu Waziri Katambi.

Awali
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba alisema
katika kipindi cha miaka sita ya uhai wa Mfuko kumekuwepo na mafanikio kadhaa
chini ya wafanyakazi 129 ambao wameweza kutekelza vema majukumu yao

“Sambamba
na hilo tumekuwa tukiwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza weledi
katika utendaji wa kazi.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Bw.
Mashomba pia alisema miongoni mwa maeneo ambayo Mfuko umeboresha sana ni kuweka
mfumo wa utoaji taarifa kwa njia ya mtandao.

“Huduma
zetu hivi sasa zinatolewa kwa kiasi kikubwa sana kwa njia ya mtandao karibu
asilimia 85 ya shughuli zetu, kujisajili, kuwasilisha michango, uchatakati wa
malipo lakini pia muhimu zaidi ni kutoa taarifa palke mfanyakazi anapougua au
kupata ajali ya kikazi na hata inapotokea bahati mbaya akafariki kutokana na
kazi tumeweka mfumo mzuri unaowezesha taarifa hizo mkutufikia kwa haraka
kupitia mtandao.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Alisema
Mfuko unatambua kuwa nchi ni kubwa na sio sehemu zote mtandao unapatikana kwa
urahisi hivyo Mfuko umefungua ofisi za kikanda, kuna ofisi Makao makuu ya Serikali
Dodoma, Mbeya, Arusha, Morogoro, Mtwara na mwisho wa mwaka huu wa fedha Mfuko
utafungua ofisi kwenye mikoa ya Tabora, Geita na Shinyanga hususan maeneo ya
migodi kama Kahama.

“Ukiacha
hayo Mfuko wetu kifedha tumejenga uwezo wa kutosha kwa mujibu wa hesabu
zilizokaguliwa na CAG tarehe 30/06/2020 tulikuwa na ukubwa wa thamani (Assets)
wa Bilioni 333, lakini pia hesabu ambazo hazijakaguliwa na CAG hadi Desemba
2020 tumefikia bilioni 389.” Alifafanua Mkurugenzi Mkuu Mshomba.
“Sambamban nahilo tumekuwa tukiwapatia mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza weledik katikautendaji wa kazi.” Alifafanua Bw. Mshomba.

Bw. Mashomba pia alisema miongoni mwa maeneo ambayo Mfuko umeboresha sana ni kuweka
mfumo wa utoaji taarifa kwa njia ya mtandao.

No comments :

Post a Comment