******************************************
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani ,linamshikilia
mtuhumiwa Shaban Athuman 61 mkazi wa Kwamakocho kata ya Mandela Chalinze
Pwani ,kwa kosa la kumiliki kiwanda cha kutengeneza silaha na vifaa vya
kutengenezea silaha za kienyeji (magobole ).
Kamanda wa polisi
mkoani Pwani,Wankyo Nyigesa ,alisema tarehe 31 majira ya usiku
alikamatwa mtuhumiwa akiwa na mtambo wa kufulia vyuma,fataki 48 na
risasi 42 za bunduki aina ya gobole.
“Pia alikutwa na
chupa 5 ndogo zenye baruti ndani yake ,paketi moja ya unga wa kiberiti
,mitambo mitatu ya silaha ambayo ipo tayari bado kuwekwa mtutu na kitako
,mitambo ya kutobolea vifaa vya miti vinavyofungwa katika silaha aina
ya gobole na kopo moja lenye unga wa tindikali ambao unatumika
kuunganisha vyuma .”
Aidha Wankyo
alieleza,alimatwa pia mtuhumiwa jina limehifadhiwa akimiliki bunduki 3
shortgun 2,na gobole moja ,risasi 13 za shortgun ,maganda 3 ya risasi
,golori 60,misumeno 2 ya kukatia mbao na chuma na kipande cha mtutu wa
bunduki .
“Amekutwa na mitambo ya kutengeneza bunduki mbili,plaizi moja ,alieleza Wankyo.
Wankyo alibainisha kuwa,juhudi za kuwatafuta watuhumiwa katika tukio hilo zinaendelea .
No comments :
Post a Comment